Alikiba Adokeza Kuachia Ngoma Mpya Mbili Hivi Karibuni

[Picha: Nairobi News]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii mashuhuri kutokea nchini Tanzania Ali Kiba amedokeza kwa mashabiki zake kuwa yuko mbioni kuachia ngoma mbili mpya hivi karibuni.

Ali Kiba ambaye wiki kadhaa nyuma alitikisa na ziara yake ya kimuziki ya ‘Only One King’ alitoa taarifa hiyo wakati akimjibu shabiki mmoja kupitia akaunti yake ya Twitter.

Soma Pia: Alikiba Afunguka Sababu ya Kutoiga Biashara ya Diamond

"When you know the UTU video is done, but you are planning to drop two bonus tracks! 2022," aliandika Alikiba kupitia akaunti yake ya Twitter kwenye ujumbe huo ambao pia ulidokeza kuwa video ya ngoma yake ya Utu pia iko tayari.

Video ya ‘Utu’ inatarajiwa kuwa video ya sita kutoka kwenye albamu ya Ali Kiba ya kuitwa ‘Only One King’ kwani kufikia sasa ameshatoa video za nyimbo kama ‘Infedele’, ‘Ndombolo’, ‘Salute’, ‘Jealousy’ pamoja na ‘Bwana Mdogo’ ambayo alimshirikisha Patoranking kutokea Nigeria.

Soma Pia: Nyimbo Tano Kutoka Tanzania Zilizozua Utata Mwaka wa 2021

Aidha, kwa siku za hivi karibuni Ali Kiba amekuwa akitumia mtandao wa Twitter kutangaza kuhusu miradi yake mipya ya kimuziki kwani siku kadhaa zilizopita kupitia akaunti ya Twitter alitangaza kuwa anafikiria kuachia albamu mpya kabisa mwaka huu wa 2022.

Ali Kiba si msanii pekee kutokea Kings Music kudokeza kuhusu ujio wa albamu kwa mwaka 2022 kwani Tommy Flavor ambaye pia ni msanii wa lebo hiyo kupitia mahojiano aliyoyafanya na mtangazaji Lil Ommy mwezi Oktoba mwaka 2021 alithibitisha kuwa yuko mbioni kuachia albamu ambayo ameipa jina la ‘Heir To The Throne’.

Leave your comment