Alikiba Afunguka Sababu ya Kutoiga Biashara ya Diamond

[Picha: Pulse Live]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mfalme wa muziki wa bongo Alikiba amefunguka kuhusu sababu ya kutoiga biashara ya msanii mwenzake Diamond Platnumz ambaye kwa siku za hivi karibuni amepamba vichwa vya habari kutokana na kampuni yake ya Wasafi Bet.

Alikiba alipotua nchini Kenya kwa ziara yake ya 'Only One King Tour', alipatana na mwanahabari ambaye alitaka kujua iwapo yeye pia anapanga kuanzisha biashara sawia. Alikiba ambaye pia ni mkurugenzi mkuu wa lebo ya Kings Music, alisema kuwa yeye hawezi ingia katika miradi kama hiyo kwani dini yake ya Kiislamu haimruhusu.

Soma Pia: Harmonize Atangaza Ujio wa Tamasha la Kusikiliza Albamu Yake ya High School

Aliongeza kuwa yeye hafahamu dini ya Diamond na hivyo basi hajui iwapo anaruhusiwa kujihusisha na biashara kama hizo.

"Unfortunately dini yangu hairuhusu, sasa sijajua dini ya Diamond," Alikiba alisema.

Alikiba vile vile katika kikao hicho na wanahabari alitoa kauli yake kuhusu kampeni iliyoanzishwa na mchekeshaji Eric Omondi ya kushurutisha vyombo vya habari kucheza 75% ya muziki wa Kenya na kisha 25% ya muziki kutoka mataifa mengine.

Soma Pia: Rosa Ree Atangaza Ujio wa Albamu Yake Mapema Mwaka Kesho

Kwa mujibu wa Alikiba, sio vyema kuweka vizuizi katika muziki kwani mwisho wa siku mashabiki wanataka kusikiliza muziki mzuri. Alikiba alisema kuwa japo ni vizuri kuupa muziki wa Kenya kipau mbele, haifai kuwekewa asilimia fulani.

Alikiba alisema kuwa kuna baadhi ya wasanii wa Kenya ambao wanafanya vizuri sana nchini Tanzania ikiwemo Otile Brown, Khaligraph Jones, Nyashinski, Sauti Sol na wengine wengi. Alikiba anatarajiwa kutumbuiza katika tamasha la Afro Vasha.

Leave your comment