Harmonize Atangaza Ujio wa Tamasha la Kusikiliza Albamu Yake ya High School

[Picha: The Standard]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii nyota kutoka Tanzania Harmonize ambaye pia ni mkurugenzi mkuu wa lebo ya Konde Music Worldwide ametangaza ujio wa tamasha la kusikiliza albamu yake ya 'High School'.

Katika kikao na wanahabari, Harmonize alisema kuwa tamasha hilo litafanyika usiku wa tarehe 31 mwezi huu wa Disemba katika eneo la Palm Village.

Soma Pia: Rosa Ree Atangaza Ujio wa Albamu Yake Mapema Mwaka Kesho

Harmonize alieleza kuwa sababu ya yeye kufanya tamasha la kusikiliza albamu yake ni kuwa wakati wa kuiachia alikuwa Marekani.

Sasa ni zamu ya mashabiki wake wa Tanzania kuja kumwona mbashara akitumbuiza nyimbo zote 20 zilizomo kwenye albamu hiyo.

"I want to make an announcement right now, niwaambie kwamba tarehe 31 ya mwezi wa 12 mkesha wa mwaka mpya basi tutakuwa na nafasi ya kufanya, au kuhudhuria kwa yeyote ambaye atakuwa nafasi ya kuhudhuria High School album launch, High School listening party ambayo itafanyika hapa Palm village," Harmonize alisema.

Harmonize aliachia albamu yake ya pili ambayo ni 'High School' wakati alikuwa kwenye ziara ya muziki nchini Marekani. 'High School' ambayo iko na ngoma ishirini zilizowaleta pamoja wasanii na watayarishaji wa muziki tofauti, imepokelewa vizuri na mashabiki na kufikia sasa imeshasikilizwa na mamilioni ya mashabiki mtandaoni.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Albamu na EP 10 Kali Zaidi Tanzania Kwa Mwaka 2021

Kando na tamasha la kusikiliza albamu yake mkesha wa mwaka mpya, Harmonize pia ametangaza ujio wa tamasha la Afro East Carnival mapema mwaka kesho.

Leave your comment