Rosa Ree Atangaza Ujio wa Albamu Yake Mapema Mwaka Kesho

[Picha: The Standard]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki nyota wa mtindo wa Hip-Hop kutoka Tanzania Rosa Ree ametangaza ujio wa albamu yake mapema mwaka kesho.

Rosa Ree aliweka tangazo hili wazi kupitia ukurasa wake wa Instagram, ambako aliashiria kuwa ako na hamu sana ya kuwapakulia mashabiki wake nyimbo zilizomo kwenye albamu hiyo.

Soma Pia: Wasifu wa Rosa Ree, Safari Yake Kimuziki, Nyimbo Zake Bora, Mahusiano na Thamani Yake

Rosa Ree, hata hivyo, hakufichua habari zaidi kuhusu albamu hiyo. Hakutaja ni ngoma ngapi zitakuwemo humo ndani au ni wasanii wagani ambao atawashirikisha.

"Whenever someone listen to my new album, can't wait to release it beginning of next year," chapisho la nyota huyo kwenye Insta Stories zake lilisomeka.

Rosa Ree ni mmoja kati ya wanamuziki wa kike nchini Tanzania ambao wamepata mafanikio makubwa sana kutokana na uwezo wao wa kurap.

Soma Pia: Rosa Ree Atofautiana na Rapa Wakazi Kuhusu Mtindo wa Hip-hop Kukosa Mvuto wa Kibiashara

Msanii huyo amesifiwa mno kwa mtindo wake wa kuimba kuhusu masuala ambayo mtu wa kawaida anapitia. Ijapo kuwa kwa siku za hivi karibuni kumekuwa na mjadala mkubwa kuhusu muziki wa Hip-Hop kufifia Tanzania, Rosa Ree anaamini kuwa mtindo huo ungali hai na wanamuziki wanafaa kujituma zaidi.

Baadhi ya wasanii tajika wa Hip-Hop ikiwemo Wakazi na Chidi Benz hivi karibuni walitoa kauli yao kuhusu sababu kuu ya muziki wa Hip-Hop kutofanya vizuri ikilinganishwa na muziki wa Bongo.

Rosa Ree kwa upande mwingine anaamini kuwa Hip-Hop bado ipo na wasanii wa mtindo huu wanapata mafanikio kama vile wasanii wa mitindo nyingine.

Leave your comment

Top stories