Rosa Ree Atofautiana na Rapa Wakazi Kuhusu Mtindo wa Hip-hop Kukosa Mvuto wa Kibiashara

[Picha: The Standard]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Rapa mwenye heshima kubwa sana Tanzania na Afrika Mashariki kwa jumla Rosa Ree ametofautiana na kauli ya rapa mwenzake Wakazi kuhusu muziki wa Hip-hop kupoteza mvuto wa kibiashara.

Rapa Wakazi kupitia ukurasa wake wa kijamii alidai kuwa chanzo cha muziki wa Hip-hop nchini Tanzania kukosa wawekezaji ni sababu yake kupoteza mvuto wa kibiashara.

Soma Pia: Wasifu wa Rosa Ree, Safari Yake Kimuziki, Nyimbo Zake Bora, Mahusiano na Thamani Yake

Alieleza kuwa muziki wa Hip-hop umekosa utaaluma na hivyo basi ni ngumu kudhaminiwa na wawekezaji.

"Tatizo tumepoteza mvuto wa kibiashara, so ni ngumu kwa wawekezaji kutudhamini. Castlelite (Which is all for Hip-hop) mwaka huu wame-base kwenye element ya DJing, instead of eMCees maana tuna lack professionalism & are losing commercial viability behind Singeli & Bongoflava," Kauli ya Wakazi mtandaoni ilisomeka.

Soma Pia: Diamond, Rayvannny, Harmonize na Wasanii Wengine Waliotazamwa Zaidi YouTube Tanzania Mwezi Novemba

Rosa Ree ametofautiana na kauli hiyo na kusisitiza kuwa muziki wa Hip-hop ungali hai na wapo marapa ambao wanapata mikataba ya kibiashara kutokana na juhudi zao.

Alieleza kuwa japo kuna mengi ambayo yanafaa kufanywa ili kuupeleka muziki wa Hip-hop kwenye hatua nyingine, sio haki kusema kuwa muziki wa Hip-hop umepoteza mvuto wa kibiashara.

"Kwa kweli hapa Wakazi sijakuunga mkono. Siamini kama haya ndio majibu yako kwa mtu ambaye anaipenda Hip Hop na kujua value yake mpaka anatamani kuwe na tamasha la Hip-hop. Kuna umuhimu wa kuona juhudi zinazofanyika na wanaHipHop out here kuweka game afloat. Ni dhahiri kwamba bado tunahitaji kufanya kazi kubwa kuweza kuikuza HipHop ila ukisema kwamba “Wana HipHop” wamekosa mvuto wa kibiashara unakosea maana wengine tunapata madili kibao," Rosa Ree alieleza.

Leave your comment