Wasifu wa Rosa Ree, Safari Yake Kimuziki, Nyimbo Zake Bora, Mahusiano na Thamani Yake

[Picha: Biggest Kaka]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Rosa Ree ni nani?

Jina la kisanii : Rosa Ree

Jina halisi: Rosary Robert Iwole

Tarehe ya kuzaliwa : April 21, 1995

Aina ya muziki : Hip-Hop

Thamani ya jumla : Haijulikani

Soma Pia: Wasifu wa Anjella, Safari Yake Kimuziki, Nyimbo Zake Bora, Mafanikio, Mahusiano na Thamani Yake

Maisha ya awali ya Rosa Ree yalikuwaje?

Rosa Ree amezaliwa huko Moshi mkoani Kilimanjaro akiwa ni mtoto wa mwisho kwenye familia ya watoto sita. Baada ya muda kupita, Rosa Ree na familia yake waliekea Kenya ambako waliishi kwa muda. Wakiwa nchini Kenya, Rosa Ree alianza elimu yake kwenye shule ya msingi ya Ainsworth pamoja na shule ya msingi ya Rudolf Steiner zote zinazopatikana jijini Nairobi. Baadaye alihitimu kwenye shule ya sekondari ya Bishop Mazzoldi.

Mara baada ya kumaliza elimu ya sekondari, Rosa Ree alikuwa na ndoto ya kwenda kusomea masuala ya dawa na uuguzi, lakini ndoto hii haikutimilika kwa kuwa wazazi wake walikuwa na upungufu wa fedha. Akiwa na miaka 18, Rosa Ree alitafuta kazi ili aweze kupata hela ya kujisomesha mwenyewe.

Rosa Ree alianza kufanya kazi kama mtu wa mapokezi kwenye kampuni moja Dar Es Salaam. Baadae akapata kazi kama mtu anayehusika na mauzo pamoja na masoko kwenye kampuni nyingine.

Soma Pia: Wasifu wa Rayvanny, Nyimbo Zake Bora, Tuzo Alizoshinda, Mahusiano na Thamani Yake

Rosa Ree alianza vipi harakati za muziki?

Baada ya kufanya kazi kwa ajili ya kujikimu kwa miezi kadhaa, shemeji yake Rosa rRee aitwaye John alimuunganisha na mtayarishaji wa muziki aitwaye ‘Mswaki’. Kutokea hapo, Rosa Ree akaanza kwenda studio za Mswaki na kujifunza zaidi kuhusu muziki wa eap na jinsi ya kupita kwenye midundo tofauti tofauti ya hip-hop.

Baada ya kuchapisha video mbalimbali kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa anarap, ndipo mkurugenzi mtendaji wa lebo ya MDB Maximillian Muniko Rioba aliona kipaji chake na kumkaribisha studioni kwake. Baada ya muda mfupi , wawili hao wakawa na ukaribu wa kikazi kiasi cha kuanza kurekodi ngoma tofauti tofauti  pamoja.

Rosa Ree alikutanaje na kundi la Navy Kenzo?

Baada ya kupikwa na kupikika chini ya Maximillian Rioba, siku moja Rosa Ree aliamua kurekodi video akiwa anaimba wimbo wa Navy Kenzo ‘Game’ na kisha kuweka video hiyo kwenye akaunti yake ya Instagram. Nahreel alipata nafasi ya kuona video hiyo  ya Rosa Ree na hapo ndipo alipata mwanya wa kufanya kazi na Navy Kenzo.

Baada ya kuwa karibu kikazi na kundi hilo, mwaka 2015 Rosa Ree alitambulishwa kama msanii rasmi wa ‘The Industry’ na akaachia ‘One Time’ kama ngoma yake ya kwanza chini ya lebo hiyo.

Nyimbo bora kutoka kwa Rosa Ree ni zipi?

  • One Time
  • Up In The Air
  • Asante Baba
  • Dip n Whine
  • Banjuka
  • That Gal
  • Kupoa
  • Watatubu
  • I'm Not Sorry

Rosa Ree ameshirikiana na wasanii gani?

Tangu aanze muziki, Rosa Ree amefanya ngoma na wasanii wengi wa ndani na nje ya nchi kama; Khaligraph Jones, Timmy Tsat, Chemical, Christian Bella, Rayvanny na wengine wengi.

Mahusiano ya Rosa Ree

Septemba 25 2021, Rosa Ree alivishwa pete ya uchumba na mpenzi wake wa muda mrefu. Ree alitumia ukurasa wake wa Instagram kufikisha taarifa hizo kwa mashabiki zake.

Leave your comment