Wasifu wa Anjella, Safari Yake Kimuziki, Nyimbo Zake Bora, Mafanikio, Mahusiano na Thamani Yake

[Picha: Anjella Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Anjella ni nani?

Jina la usanii : Anjella

Jina Halisi: Angelina George Samson

Tarehe ya kuzaliwa: Oktoba 3, 2000

Aina ya mziki: Bongo Fleva

Thamani ya jumla: Haijulikani

Maisha ya awali ya Anjella yalikuwaje?

Anjella ni mtoto wa mwisho kwenye familia ya watoto watatu. Asili yake ni huko mkoani Tabora, lakini akiwa mtoto aliishi mkoani Tanga kwa muda kisha baadae, wazazi wake wakahamia mkoa wa Dar es salaam maeneo ya Kimara Bonyokwa. Hapo ndipo wanaishi mpaka sasa.

Anjella amehitimu elimu ya shule msingi mwaka 2013 na ilipofika mwaka 2017 alihitimu elimu ya sekondari kwenye shule ya King'ongo, Dar es salaam.

Ni wazi kuwa kipaji cha kuimba cha Anjella kimechagizwa sana na wazazi wake ambao walikuwa wanaimba kwaya kanisani. Hii ilipelekea mwanadada huyu kulelewa kwenye mazingira ya dini sana kiasi cha kuanza kuimba kwaya kanisani akiwa mdogo.

Soma Pia: Wasifu wa Rayvanny, Nyimbo Zake Bora, Tuzo Alizoshinda, Mahusiano na Thamani Yake

Anjella alianzaje kazi zake za muziki na lini?

Anjella alianza kuimba akiwa darasa la nne. Mara tu alipomaliza kidato cha nne mwaka 2017, akaanza kuzunguka studio mbalimbali  akitafuta nafasi ya kurekodi nyimbo zake.

Akiwa kwenye harakati hizo, siku moja akiwa anaangalia TV akaona mashindano ya kuimba ya kuitwa ‘Club Raha Leo’ yanayoandaliwa na kituo cha TBC na Anjella hakufanya ajizi akaamua kushiriki. Kupitia mashindano hayo ndipo alianza kuamini kuwa ana kipaji baada ya majudge kumsifia kuwa anajua sana kuimba.

Anjella alishika nafasi ya nne kwenye mashindano hayo. Japo hakushinda shindano hilo la ‘Club Raha Leo’, alipata mawasiliano (connection) na studio mbalimbali za kurekodi ngoma. Kutokea hapo, Anjella alizidi kuzunguka studio mbalimbali kwa ajili ya kurekodi covers za wasanii wakubwa. Kuna kipindi ilimlazimu kuimba sokoni au sehemu zenye watu wengi ili aweze kupata nauli za kuhudhuria studio na kulipia vifaa vya studio.

Soma Pia: Wasifu wa Rosa Ree, Safari Yake Kimuziki, Nyimbo Zake Bora, Mahusiano na Thamani Yake

Anjella Alikutana vipi na Harmonize?

Wanasema mgaa gaa na upwa hali wali mkavu. Baada ya kurekodi video nyingi akiwa anaimba cover za wasanii tofauti tofauti, siku moja Harmonize alitumiwa video ya Anjella akiwa anaimba,  kwa njia ya Whatsapp. Harmonize alikoshwa sana na kipaji cha Anjella na akaamua kupost video ya hiyo ya Anjella kwenye akaunti yake ya Instagram.

Baada ya kupost video hio, Harmonize alifahamu ukurasa wa Anjella wa Instagram na akamtumia ujumbe (DM) kuwa anaomba Anjella ashiriki kwenye ngoma yake. Baada ya hapo, Harmonize na Anjella walikutana na wiki chache baadae, Anjella akatambulishwa kama msanii rasmi wa Konde Gang.

Nyimbo Bora Za Anjella ni zipi?

  • Kama ft Harmonize
  • Si Saizi Yako & AT
  • Nobody
  • Sina Bahati

Mafanikio Ya Anjella Kwenye Muziki Ni Yapi?

Anjella kufikia sasa ana wafuasi takriban laki tano kwenye ukurasa wake wa Instagram. Mwezi Juni mwaka huu, Anjella alitunukiwa tuzo ya ‘Silver Plaque’ na YouTube baada ya kufikisha subscribers laki moja kwenye akaunti yake.

Aidha, video ya Anjella ya ‘Nobody’ iliyotoka mwezi Mei mwaka huu ilimuweka kwenye ramani nzuri baada ya kufikisha watazamaji milioni moja ndani ya siku moja pekee.

Mahusiano ya Anjella

Anjella mara zote amekuwa akipendelea kuweka mahusiano yake binafsi. Kufikia sasa, hajawahi kumuweka wazi mpenzi kwenye mitandao ya kijamii au vyombo vya habari.

Leave your comment