Maua Sama Aweka Wazi Mipango ya Kufungua Lebo Yake ya Muziki

[Picha: YouTube]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki anayefanya vizuri kwenye soko la muziki nchini Tanzania Maua Sama hivi karibuni ameweka matamanio yake ya kuanzisha lebo au kampuni yake mwenyewe ya kusimamia wasanii.

Akizungumza na Lil Ommy, Maua Sama alisema kuwa muda sahihi ukifika anatamani kuwa na lebo yake mwenyewe.

Soma Pia: Maua Sama Aeleza Maoni Aliopata Kutoka kwa Mwana Fa Kabla ya Kutoa Ngoma ya ‘Zai’

"I think kwa sababu hata mimi mwenyewe nina experience ya muziki i think its time hata mimi mwenyewe nianzishe lebo yangu. Maybe I just need a little bit time. I think its time na mimi nitafte wasanii wangu," alizungumza Maua Sama.

Kiu na hamasa ya Maua Sama kuwapa nafasi wasanii wachanga ilionekana miaka michache nyuma baada ya Sama kumshirikisha Hanstone ambaye kipindi hicho alikuwa hajulikani kabisa kwenye ngoma ya ‘Iokote’ ambayo iliweza kutetemesha kiwanda cha muziki nchini Tanzania.

Soma Pia: Maua Sama Atangaza Rasmi Kuachia Ngoma Mfululizo

Kuhusu sababu ya kumshirikisha Hanstone kwenye ‘Iokote’, Maua Sama alieleza kuwa hakufanya ajizi kumshirikisha Hanstone ambaye alikuwa ni msanii mdogo sana, kwenye ngoma ya "Iokote" kwani hata yeye wakati anaanza muziki aliaminiwa na Mwana FA na kufanya nae ngoma ya pamoja.

“Kama mimi nilipata nafasi sijulikani, nikapata nafasi ya msanii kama Mwana FA kuniweka kwenye wimbo ni nafasi tosha ya mimi sasa hivi niweze kumtoa Hanstone na nilivyofanya hivyo watu wakaafiki na here we are," alizungumza Maua Sama.

Kama Maua Sama ataamua kuanzisha lebo yake mwenyewe, basi atakuwa ni kati ya wasanii wachache bongo ambao walishawahi kumiliki lebo zao wenyewe, kwani Vanessa Mdee nae miaka michache nyuma alianzisha Mdee Music lebo ambayo ilikuwa inasimamia kazi za Brian Simba pamoja na Mimi Mars.

Leave your comment