Maua Sama Atangaza Rasmi Kuachia Ngoma Mfululizo

[Picha: Maua Sama Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Malkia wa muziki wa bongo Maua Sama ametangaza rasmi kwamba kwa sasa amechukua mfumo wa kuachia ngoma mfululizo.

Kupitia taarifa aliyochapisha kwenye ukurasa wake wa kijamii, msanii huyo alisema kuwa amepokea malalamishi kutoka kwa mashabiki wake baada ya kutoa ngoma ya 'Baba Jeni'.

Soma Pia: Ray C Aomba Serikali Kuingilia Kati Ugomvi Uliopo Baina ya Harmonize na Diamond

Malalamishi hayo yalitokana na sehemu ya mashabiki wake kutoelewa sababu ya Maua kutoa ngoma mpya wakati ngoma yake ya 'Zai' bado inavuma mtandaoni na haijamaliza hata miezi miwili.

Maua alifafanua kuwa huo ndio mtindo wake mpya wa kuachia ngoma mfululizo. Maua Sama aliomba radhi kwa mashabiki wake ambao hawajazoea mfumo huo wa kuacha muziki.

Soma Pia: Video ‘Inama’ ya Diamond Platnumz na Fally Ipupa Yafikisha Watazamaji Milioni 100

Vile vile, malkia huyo alipigia kampeni ngoma yake mpya ya 'Baba Jeni' kwa kuwashawishi mashabiki wauskilize katika jukwaa tofauti za kusikiliza muziki kwenye mtandao.

"Napokea malalamiko mengi kwanini Baba jeni ametoka wakati Zai ina Mwezi to mtaani. Naomba kuwajulisha, Hii staili yakutoa ngoma inaitwa "uzazi wa mpango wa muziki" Yani mtoto akienda Mjini namleta mwengine. Naomba mnivulimie kwa usumbufu wowote utakaojitokeza Kwenye kupanga Playlist zenu. Enjoy Good Music," ujumbe wa Maua Sama mtandaoni ulisomeka.

Hapo awali kabla ya kuachia ngoma yake ya 'Zai', Maua Sama alimshirikisha rapa Young Lunya kwenye ngoma ya 'Away'. Ngoma hizo mbili zilipata mapokezi mazuri haswaa 'Zai' ambayo imetazamwa takriban mara laki saba kwenye mtandao wa YouTube.

Maua Sama ni mmoja kati ya wanamuziki wa kike ambao wanavuma sana kwenye tasnia ya muziki wa Tanzania.

Leave your comment