Video ‘Inama’ ya Diamond Platnumz na Fally Ipupa Yafikisha Watazamaji Milioni 100

[Picha: CitiMuzik]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki kutokea nchini Tanzania Diamond Platnumz ameweka rekodi mpya baada ya video ya ngoma yake ya ‘Inama’ aliyofanya na Fally Ipupa kutazamwa mara milioni mia moja kwenye mtandao wa YouTube.

Video ya ‘Inama’ ilitoka Juni 9 mwaka 2019, hivyo imetumia takribani miaka miwili na miezi mitano kufikisha idadi hiyo ya watazamaji.

Soma Pia: Rayvanny Adokeza Ujio wa Wimbo Mpya na Maluma Baada ya Kuachia ‘Mama Tetema’

Video hii iliongozwa na Director Kenny ambaye kipindi hicho alikuwa chini ya kampuni ya Zoom Extra ambayo inamilikiwa na Diamond Platnumz.

Kumshirikisha Fally Ipupa ambaye ni moja ya wasanii wenye mashabiki wakubwa sana Afrika Mashariki na kati ni moja ya sababu iliyochagiza video kutazamwa zaidi, kwani wengi walikuwa na shauku ya kumuona Diamond Platnumz na Fally Ipupa kwa pamoja.

Aidha, maudhui ya video kuanzia miondoko na mitindo ya kucheza, ubora wa picha pamoja na ubunifu uliotumika umefanya video hii kupata watazamaji wengi.

Soma Pia: Serikali ya Tanzania Yampongeza Rayvanny Kwa Kuandikisha Historia Kwenye Tuzo za MTV EMA 

Video ya ‘Inama’ ni video ya pili kutoka kwa Diamond Platnumz kufikisha watazamaji milioni mia moja kwenye mtandao wa YouTube. Video yake ya kwanza ilikuwa ni ‘Yope Remix’ ambayo alifanya na Innos B ambaye pia alitokea Congo.

Rekodi hii kutoka kwa Diamond Platnumz imezidi kumuweka msanii huyo kama kinara wa YouTube nchini Tanzania.

Ngoma zake zingine kama ‘Waah’ aliyofanya na Koffi Olomide na ‘Nana’ ambayo ameshirikiana Mr Flavour kutokea Nigeria pia zinafanya vyema kwenye mtandao huo.

https://www.youtube.com/watch?v=x96N7f62GE4

Leave your comment