Ray C Aomba Serikali Kuingilia Kati Ugomvi Uliopo Baina ya Harmonize na Diamond

[Picha: All Africa]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki mkongwe wa Bongo Ray C ameiomba serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuingilia kati ya uhasama uliopo baina ya wasanii wawili wakubwa nchini humo.

Kupitia ujumbe aliouchapisha mtandaoni, Ray C alisema kuwa vita vinavyoshuhudiwa kati ya wasanii hao ambao hakuwataja kwa majina, huenda vikawa na mwisho mbaya.

Soma Pia: Harmonize Aeleza Kwa Upana Sababu ya Mgogoro Baina Yake na WCB

Kwa mujibu wa Ray C, ugomvi huo unawachafulia wasanii hao picha na iwapo hakuna yeyote atakayeingilia kati, basi kuna uwezekano kuwa mwisho wake ukawa mauti.

Ray C alikuwa akizungumza muda mfupi baada ya msanii nyota Harmonize kufunguka kuhusu visa vilivyomsukuma hadi akatoka WCB.

Harmonize vile vile alifchua mambo mengi ambayo mashabaki hawakuwa wanafahamu kuhusu uhusiano wake na lebo hiyo. Malkia huyo wa muziki wa bongo aliwashauri watanzania kutofurahia vita vya wasanii hao bali kuketi chini na kujaribu kusuluhisha ugomvi huo.

Soma Pia: Rayvanny Adokeza Ujio wa Wimbo Mpya na Maluma Baada ya Kuachia ‘Mama Tetema’

Alisisitiza kuwa ugomvi huo uliikuwa umezidi bifu za kawaida ambazo hushuhudiwa miongoni mwa wasanii.

"Kwenye muziki beef za hapa na pale zipo ila hii ni zaidi ya beef, hii ni vita moja kubwa ya kushushana na kuharibiana brands, na nasema hili kwa pande zote mbili, sio kitu cha sisi watanzania kukifurahia hata kidogo kama kweli tunawakubali kwa moyo mmoja wasanii hawa. Hawa ndio wanaopeperusha bendera kwa sasa bila ubishi," kipande cha ujumbe wa Ray C mtandaoni kilisomeka.

Leave your comment