Harmonize Aeleza Kwa Upana Sababu ya Mgogoro Baina Yake na WCB

[Picha: Ghafla]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki Harmonize kwa mara ya kwanza ameelezea kwa undani sababu za kuwepo kwa mgogoro kati yake na lebo iliyokuwa inasimamia kazi zake zamani ya WCB.

Kwa siku za hivi karibuni, kupitia mitandao ya kijamii kumekuwa na vita vya maneno baina ya Harmonize na Diamond Platnumz.

Soma Pia: Harmonize Aibua Maswali Baada ya Kuwa 'Unfollow' Wasanii wa Tanzania Kwenye Instagram

Wiki kadhaa nyuma, watu mbalimbali maarufu ambao mara nyingi huonekana kuiunga mkono lebo ya WCB, walionekana kumdhihaki msanii huyo kutokana na maonesho yake ya nchini Marekani kuhudhuriwa na watu wachache.

Akizungumza muda mfupi mara baada ya kutua Tanzania kutokea nchini Marekani, Harmonize alidai kuwa kwenye mkataba wake na WCB, alikuwa anapata asilimia 40 tu huku lebo hiyo ikichukua asilimia 60 ya mapato yake yote.

Soma Pia: Harmonize Akataa Kulinganishwa na Msanii Yeyote, Aapa Kuibadilisha Tasnia ya Muziki

Harmonize alisema kuwa aliamua kuondoka kwenye lebo hiyo baada ya baadhi ya watu kujaribu kumfarakanisha yeye na Diamond Platnumz kitu kilichopelekea Harmonize kuanza kuwekewa vikwazo na changamoto kipindi akiwa ndani ya lebo hiyo.

"Wakawa wanasema si umeona Dogo anataka kushindana na wewe. Hiyo bro wangu (Diamond Platnumz) akaibeba. Na mimi hata leo nilivyo Harmonize anavaa macheni lakini baba yangu siwezi kumbadilisha. Kwa hiyo baba angu alivyokuwa akinitembelea nyumbani wakawa wanasema baba angu amekuja kumroga Diamond.

Kwa hiyo siku hadi siku vikawa vitu vingi vinakuja ikawa sasa kama natafutiwa sababu niweze kuondoka," Harmonize alidai.

Kulingana na Harmonize, baada ya kuona hawezi kuendelea kuwa chini ya WCB aliomba kusitisha mkataba wake na alitakiwa kulipa kianzio cha Milioni 300 ili aweze kuondoka kwenye lebo hiyo.

Leave your comment