Harmonize Aibua Maswali Baada ya Kuwa 'Unfollow' Wasanii wa Tanzania Kwenye Instagram

[Picha: Ghafla]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii maarufu kutoka Tanzania Harmonize amekua gumzo mtandaoni kutokana na hatua yake ya kuwa 'unfollow' wanamuziki wa bongo.

Hatua hiyo imeibua maswali mengi miongoni mwa wadau tofauti kwenye tasnia ya muziki Tanzania. Kutokana na ukubwa alionao si Tanzania tu bali barani Afrika nzima, hatua hiyo imesababisha mjadala mkubwa kuhusu umoja na uungaji mkono baina ya wasanii.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Harmonize Aachia Video ya Ngoma Yake Mpya ‘Outside’

Harmonize alijitetea kwa kusema kuwa yeye kuwa 'unfollow' wanamuziki wenzake wa bongo hakukua kwa nia mbaya na bado anawaheshimu na kutii kazi zao.

Harmonize, hata hivyo, aliwabakisha wasanii wanne tu wa bongo ambao hakuwa 'unfollow', nao ni; Mr. Blue, Professor Jay, Aslay na Lady Jaydee.

Harmonize, vile vile, alipunguza idadi ya watu ambao alikuwa amewafuata kwa jumla kwenye ukurasa wake wa Instagram kutoka 900 hadi 289.

Soma Pia: Harmonize Akataa Kulinganishwa na Msanii Yeyote, Aapa Kuibadilisha Tasnia ya Muziki

"I love everybody out there but I just wanna follow the woman of my life so don't feel like I don't love and respect you after unfollow you mean a lot to me life," ujumbe wa Harmonize mtandaoni ulisomeka.

Hatua hii inatokea siku chache tu baada ya Harmonize kupamba vichwa vya habari kwa kusitisha kumfuata staa wa muziki na pia mkurugenzi mkuu wa lebo ya WCB Diamond Platnumz. Hatua hii ilisababisha gumzo mtandaoni haswaa ikizingatiwa kuwa Diamond Platnumz alihusika pakubwa katika kumjenga Harmonize na kumpa umaarufu kupitia lebo ya WCB kabla ya tofauti kuibuka baina yao.

Leave your comment