Maua Sama Aeleza Maoni Aliopata Kutoka kwa Mwana Fa Kabla ya Kutoa Ngoma ya ‘Zai’

[Picha: Citi Muzik]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki Maua Sama ameweka wazi namna ambavyo rapa kutokea nchini Tanzania Mwana FA alimpa changamoto wakati yuko kwenye hatua za mwisho kabisa kutoa ngoma yake inayobamba Tanzania kwa sasa ‘Zai’.

Akiongea kwenye mahojiano aliyoyafanya hivi karibuni, Maua alisema kuwa siku kadhaa kabla ya kuachia ngoma ya ‘Zai’ alimtumia ngoma hiyo Mwana FA ili atoe maoni yake, lakini rapa huyo kwa upande wake hakuona kama ‘Zai’ ni ngoma nzuri, kitu ambacho kilimhuzunisha Maua Sama.

Soma Pia: Maua Sama Atangaza Rasmi Kuachia Ngoma Mfululizo

"Sasa nikamtumia wimbo ‘Zai’ (Mwana FA) nikamwambia brother huu vipi? Akaniambia its an okay song, I don't know si ufeel kama ni wimbo mzuri. Nikamjibu kweli? Akasema sawa," alizungumza Maua Sama.

Maua alizidi kudokeza kuwa kwa upande wake pamoja na Mwana FA kutopitisha ngoma hiyo, aliamua kuiachia kwa mashabiki zake kwani kwake yeye Zai ilikuwa ni ngoma kali sana.

Soma Pia: Maua Sama Azungumzia Uhusiano Wake Na Nandy

"But still my heart was moving me kutoa Zai, moyo wangu ukawa unataka kweli nitoe Zai. This time around kusema ule na ukweli nimevunja kabisa masharti ya the way nnavyotaka kufanya muziki wangu toka nilivyokuwa namsikiliza brother (Mwana FA) nikasema ngoja tutoe. Then nikaongea na Manager tukatoa without his concern," aliweka bayana Maua Sama.

Tangu kuachiwa kwake mwezi Septemba mwaka huu, ‘Zai’ imekuwa ni ngoma pendwa sana kwa mashabiki wa muziki na kufikia sasa video ya wimbo huo imeshatazamwa mara laki saba tisini na nne kwenye mtandao wa YouTube.

Leave your comment