Lava Lava Adokeza Ujio wa Ngoma yake Mpya 'Desh Desh'

[Picha: Lava Lava Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Nyota wa muziki wa bongo Lava Lava amedokeza ujio wa ngoma mpya hivi karibuni. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Lava Lava alifichua maudhui ya wimbo huo na kunukuu mistari kadhaa.

Kwa mujibu wa chapisho hilo, ngoma hiyo inatarajiwa kuwa ya mapenzi. Hii inatarajiwa kuendeleza mafanikio ya msanii huyo ambaye kwa siku za hivi karibuni ameonekana kufanikiwa sana na ngoma zake zinazo husu mapenzi.

Soma Pia: Ibraah Adhibitisha Kukamilika kwa Albamu Yake

Kwenye chapisho hilo, msanii huyo ambaye amesainiwa katika lebo ya WCB, alimshukuru Mungu kwa kumuezesha kukamilisha ngoma hiyo. Lava Lava alionekana mwenye hamu kubwa kuiachia kazi hiyo kwa mashabiki wake.

"God is good thank you so much guys new chocolate sound on de way #deshDesh Eti jamani mtu uliekuwa nae kwasasa kimahusiano uko tayari kututajia au ndo deshi deshi ....... Unamficha hutaki watu wamjue?" Chapisho la Lava Lava lilisomeka.

Soma Pia: Whozu Atangaza Kuachia Albamu Mwaka Huu

Kwenye chapisho lingine, Lava Lava alionekana mwingi wa matumaini kuwa ngoma hiyo iliyopewa jina la ‘Desh Desh’ itapata mapokezi mazuri kutoka kwa mashabiki wake.

"Jamani hii Desh Desh inaniwasha kila nikiskiza napata picha kabisa wadada uko tiktok watakavyojishauwa," chapisho lingine la Lava Lava lilisomeka.

Hapo awali, Lava Lava aliachia ngoma ya ‘Ng'ari Ng'ari’ ambayo ilifanya vizuri sana. Na kabla ya hapo, alikuwa ameachia ‘Inatosha’ ambayo pia ilivuma mtandaoni. Je, ‘Desh Desh’ itaendeleza moto wa Lava Lava?

Leave your comment