Nyimbo Mpya: Zuchu Aachia Video ya ‘Mwambieni’

[Picha: Ghafla]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Nyota wa muziki kutoka Tanzania Zuchu ameachia video ya ngoma yake pendwa ya ‘Mwambieni’.

Video ya ‘Mwambieni’ inakuja takriban wiki mbili tangu audio ya wimbo huo itoke. Tangu kuachiwa kwake, ngoma hiyo imekuwa ni ngoma pendwa ikisikika sehemu mbalimbali hapa nchini Tanzania.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Kusah Aachia Ngoma Mpya ‘Pain Killer’ Akiwashirikisha Kataleya & Kandle

Video ya ‘Mwambieni’ imeundwa na stori nzuri ambayo inaanza kwa kumuonesha Zuchu akiwa mbele za watu kwenye mitaa ya uswahilini akiimba kuhusu jinsi mpenzi wake wa zamani anavyohangaika kumrudia.

Ubunifu mkubwa umetumika katika kutengeneza video hii kwani mandhari yaliyotumika, namna ya kuchukua video pamoja na mavazi aliyovaa Zuchu kwenye video hii yanaakisi mtindo wa maisha wa miaka ya 1980 na 1990.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Saraphina Aachia Ngoma Mpya ‘Wamerudiana’

Aidha, uamuzi wa Zuchu kumtumia mchekeshaji Jay Mondy kwenye video hii ni wa kupigiwa makofi kwani uwepo wa mchekeshaji huyo umeleta uhalisia kutokana na uwezo wake mkubwa wa kuchekesha aliouonesha kwenye kazi hii.

Director Hanscana ndiye aliyeshikilia usukani kuongoza video hii ambayo ni ya pili kufanya na Zuchu, ya kwanza ikiwa ni ‘Nyumba Ndogo’ ambayo iliachiwa Julai mosi mwaka 2021.

‘Mwambieni’ ni video ya kwanza kutoka kwa Zuchu kwa mwaka 2021 na ni video inayotarajiwa kuweka rekodi mbalimbali kwa mwaka huuu kwa upande wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=j3kDvCgCG0Y

Leave your comment