Nyimbo Mpya: Saraphina Aachia Ngoma Mpya ‘Wamerudiana’

[Picha: Nyimbo Mpya]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Nyota wa muziki kutoka Tanzania Saraphina ameachia ngoma mpya ambayo ameipa jina la ‘Wamerudiana’.

Saraphina ambaye alipata umaarufu kupitia shindano la kusaka vipaji la Bongo Star Search anaachia ngoma hii ikiwa imeshatimia miezi takriban miwili tangu aachie ngoma yake ya ‘Pekecha’.

Pakua Ngoma za Saraphina Bila Malipo Kwenye Mdundo

‘Wamerudiana’ ni ngoma yenye vionjo vya Baibuda yaani mchanganyiko kati ya Bongo Fleva na Taarab. Ndani ya ngoma hii, Saraphina analalamika kwani mpenzi wake amemuacha yeye na kumrudia mpenzi wake wa zamani.

"Ulinidanganya mi wa kufa kuzikana nami nikazama kukupenda baba ye si ndo alofanya ukalia sana moyo ukaugawanya mbona mmerudiana?" anaimba Saraphina kwenye aya ya kwanza ya ngoma hii.

Soma Pia: Diamond, Harmonize na Wasanii Wengine Waliotazamwa Zaidi YouTube Tanzania Januari 2022

Huu ni wimbo ambao umebeba ujumbe mzito sana wa mapenzi hasa kwenye kipindi hiki tunachoelekea Valentines. Bila shaka hujawahi kumsikia Saraphina akiimba kwa hisia, utulivu na kwa huzuni kama kwenye ngoma hii.

Kazi hii ya kipekee kutoka kwa Saraphina imetayarishwa na Aloney M mtayarishaji wa muziki kutoka Tanzania ambaye pia amehusika kuandaa wimbo wake Ruby ya kuitwa ‘Sesa’.

Pia ameshashiriki kuandaa ngoma za wasanii wakubwa kutoka Tanzania kama vile Nedy Music, Christian Bella, Winnie pamoja na Ben Pol.

‘Wamerudiana’ ni wimbo wa kwanza wa Saraphina kwa mwaka huu na muda si mrefu huenda akaachia video ya ngoma hii.

https://www.youtube.com/watch?v=_iYZphrap7U

Leave your comment

Top stories

More News