Nyimbo Mpya: Kusah Aachia Ngoma Mpya ‘Pain Killer’ Akiwashirikisha Kataleya & Kandle

[Picha: YouTube]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Staa wa muziki kutoka Tanzania Kusah ameachia ngoma mpya aliyoipa jina la ‘Pain Killer’.

Kwenye ‘Pain Killer’, Kusah ameshirikiana na kundi la muziki kutokea nchini Uganda la kuitwa Kataleya and Kandle.

Pakua Nyimbo Zake Kusah Bila Mlaipo Kwenye Mdundo

Ndani ya ngoma hii, Kusah anakiri mahaba aliyonayo kwa mpenzi wake na anaonesha ni jinsi gani anatamani kumuoa na kuishi pamoja na mpenzi wake huyo ambaye amempa jina la Painkiller.

"Niko hapa nawaza nikupendeje kwemye harusi yetu sisi baby tuweje. I wish to love you forever twende popote wherever we Adam mi Eva. Sweet like a pineapple kwako naonja pepo. Hupelekwi na upepo nimefika kunako" wanaimba kwenye aya ya kwanza.

Utamu wa ngoma hii umenogeshwa zaidi na sauti tamu ya wanadada Kataleya na Kandle ambao kwa umoja wao wameimba kwa kutumia lugha tatu ambazo ni kiswahili, kiingereza pamoja na kiganda.

Ngoma hii imetayarishwa na Cukie Dady mtayarishaji wa muziki ambaye pia amehusika kutayarisha kazi nyingine za Kusah kama ‘I Wish’ pamoja na ‘I Don't Care’

Pia ameshafanya kazi na wasanii wakubwa kutoka Tanzania kama Christian Bella pamoja na Rapcha hasa kwenye albamu yake ya ‘Wanangu 99’.

Kataleya & Kandle ni akina nani?

Kataleya na Kandle ni kundi la muziki kutoka nchini Uganda ambalo limeundwa na wasichana wawili ambao ni Kataleya, pamoja na Kandle.

Wanadada hao walitoa ngoma yao ya kwanza kubwa Julai 9 mwaka 2021 ya kuitwa ‘Muzibe wa Love’.  Tangu hapo, wamekuwa wakitoa ngoma tofauti tofauti kama vile ‘Do Me’ na ‘Tonaffya’ ambazo zimefanya vizuri nchini Uganda.

Kwa sasa kundi hili ni moja kati ya makundi ya muziki yanayofanya vizuri sana nchini Uganda. mwezi Desemba mwaka 2021, walishinda tuzo yao ya kwanza ya Patiwan Awards kama wasanii chipukizi upande wa wanawake huko nchini Uganda.

https://www.youtube.com/watch?v=l5dnj8_wP3g

Leave your comment

Top stories

More News