Nyimbo Mpya: Dully Sykes Aachia Ngoma Mpya ‘Unanipagawisha’

[Picha: Nyimbo Mpya]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwana muziki wa Bongo Fleva Dully Sykes ameachia wimbo mpya kwa jina ‘Unanipagawisha’.

Kwenye ‘Unanipagawisha’, Dully Sykes anaonesha ni kwa namna gani huba kutoka kwa mpenzi wake limemnogea kiasi cha kuhisi kabisa kuwa mpenzi wake ‘anampagawisha’ na kuhisi kurukwa akili.

Pakua Nyimbo za Dully Sykes Bila Mlaipo Kwenye Mdundo

“Unanipagawisha unanipa presha mama washatukosanisha, wakutupatanisha nani. Tukizikutanisha unahakikisha mama unahakikisha kila siku napata raha ya maisha. Ninapenda unavyoiweza unavyoishika. Napenda ukinishika unavyoinama unanipagawishi," anaimba Dully Sykes kwenye aya ya kwanza.

Uzuri wa ngoma hii unatokana na mashairi yake kuwa rahisi kuimbika na pia mdundo mwepesi ambao umetumika umefanya ngoma hii kutoka kwa Dully Sykes kuwa kali sana.

Ngoma hii imepikwa Dhahabu Records studio ambayo iko chini ya Dully Sykes ambaye amehusika kutayarisha ngoma hii akiwa na mtayarishaji wa muziki wa kuitwa Tony Drizzy ambaye pia ametayarisha ngoma ya ‘Shuka La Masai’ ya Moni Centrozone inayopatikana kwenye Road to Mazengo.

Ngoma hii inakuja takriban miezi mitatu tangu aachie ngoma yake ya kuitwa ‘Nani’ ambayo pia iliweza kufanya vizuri sana hapa nchini Tanzania.

https://www.youtube.com/watch?v=yQHsVUh3lQ0

Leave your comment