Harmonize Atangaza Wasanii Watakaotumbuiza Kwenye Tamasha Yake ya Afro East Carnival

[Picha: The New Times]

Mwandishi: Omondi otieno

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii tajika kutoka Tanzania Harmonize ametangaza majina ya wasanii watakaotumbuiza kwenye tamasha yake ya Afro East Carnival mwezi Machi mwaka huu.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Harmonize alitangaza orodha ya wasanii thelathini na nne na kuongeza kuwa wasanii wengine watatangzwa baadaye.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Jux ‘I Love You’, Maua Sama ‘Shukurani’ na Nyimbo Zingine Mpya Zilizoachiwa Wiki Hii

Wasanii waliotangazwa kwenye orodha ya kwanza ni kama vile; Eddy Kenzo, Marioo, Skales, Otile Brown, Dayna Nyange, Ibraah, Sat B, John Frog, Big Fizzo, Fik Fameica na Anjella.

Wengine ni kama vile; Bruce Melodie, Amber Lulu, Varednegu, Ben Pol, Mabantu, Killy, Saraphina, Cheed, Stamina, Kusah, MC Balaa, AT, Sholo Mamba, Kinata MC, Barnaba, Dulla Makabila, Moni Centrozone, Baddest, Kayumba na Maarifa.

Soma Pia: Video ya ‘Waah’ ya Diamond Platnumz Yafikisha Watazamaji Milioni 100

Wasanii wanaotamatisha orodha hio ni; Awilo Longomba, Lody Music na Mzee wa Bwax.

Tamasha hio inatarajiwa kufanyika kwa siku tatu kuanzia Machi tarehe 5 hadi tarehe nane.

Hii inatarajiwa kuwa tamasha la kwanza kufanyika kwa siku tatu mfululizo nchini Tanzania.

Leave your comment