Zuchu Akana Kutumia Maneno Machafu Kwenye Mahojiano
14 January 2022
[Picha: The Citizen]
Mwandishi: Brian Sikulu
Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram
Malkia wa muziki wa bongo Zuhura Othman Soud, almaarufu Zuchu, amekana vikali madai kuwa alitumia lugha chafu katika mahojiano aliyoyafanya mwaka jana na mtangazaji Aaliyah.
Baada ya video tata kusambaa mtandaoni ya msanii huyo, hatimaye alitoa taarifa akieleza chanzo cha video hiyo huku akiwashauri wafuasi wake kuipuuza.
Soma Pia: Meneja wa Nandy Azungumzia Madai ya Bifu Kati ya Nandy na Wasafi
Kwenye video husika, sauti inayotuhumiwa kuwa ya Zuchu inasikika ikisema maneno ambayo hayaandikiki wala kusemeka hadharani. Zuchu hata hivyo amesema kuwa video hiyo imefanyiwa upotoshaji na sauti iliyotumika sio yake.
Alieleza maneno halisi aliyoyatumia na kusisitiza kuwa kamwe hawezi akasema maneno kama yale aliyokuwa ametuhumiwa kusema. Aidha, Zuchu aliomba radhi kwa walioathirika kutokana na upotoshaji huo.
Soma Pia: Rayvanny ‘Rara’, Christian Bella ‘Teamo’ na Nyimbo Zingine Mpya Tanzania Wiki Hii
Aliongeza kuwa yeye ni msanii aliyesajiliwa na BASATA na hivyo basi aneelewa sheria ambazo mwanamuziki anafaa kutii moja wapo ikiwa kutumia lugha ya heshima kwa jamii.
"Habari! Siku hizi za Karibuni nimekua nikiona hii video ya mahojiano tuliyofanya mwaka jana mimi Na Mtangazaji @thisisaaliyaah ikisambaa na watu wachache wakijaribu kupotosha maana ya mazungumzo yaliyofanyika .Neno nililotumia Hapo Ni neno “Mtambo “ mi ni msanii niliesajiliwa na @basata.tanzania Hivo najua kanuni na sheria elekezi," Zuchu aliandika mtandaoni.
"Pia ni balozi ninaewakilisha Taasisi Kubwa kwa akili yangu timamu siwezi kutumia lugha yoyote ya matusi ya wazi kwenye Chombo cha habari .Niombe radhi na nitoe pole kwa jamii na mashabiki zangu wote mliokereka na upotoshaji huu .Na naomba Mpuuzie upotoshaji huu Unaoendelea," taarifa yake Zuchu iliendelea kusomeka.
Leave your comment