Rayvanny ‘Rara’, Christian Bella ‘Teamo’ na Nyimbo Zingine Mpya Tanzania Wiki Hii

[Picha: YouTube]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Kama unapenda muziki kutokea nchini Tanzania pasi na shaka wiki hii imekuwa njema sana kwako kwani watanzania wameendelea kuachia ngoma kali ambazo zimelenga kuwaburudisha mashabiki. Zifuatazo ni ngoma tano mpya kutoka Tanzania ambazo zimeingia sokoni kwa wiki hii:

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Rapa Joh Makini Aachia Ngoma Mpya ‘Brand’

I Dont Care - Kusah

Baada ya ‘I Wish’ kutikisa kila kona ya Tanzania, wiki hii Kusah aliachia kibao chake kipya kabisa cha kuitwa ‘I dont care’.  Ndani yake anaonesha ni kwa namna gani anampenda kwa dhati mpenzi wake kiasi cha kutaka kumpatia dunia. Kufikia sasa imeshatazamwa takriban mara laki moja thelathini na tano kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=Njlf7Ip8G94

Rara - Rayvanny

‘Rara’ ni video ya kwanza ya Rayvanny kwa mwaka 2022 na bila shaka mashabiki wengi wameonekana kuvutiwa na kazi hii kutokana mashahiri yake mepesi na rahisi kuimbika.

https://www.youtube.com/watch?v=qVo459zuKgo

Teamo - Christian Bella ft CBO

Mwanamuziki Christian Bella amezidi kuonesha ufundi wake katika kuandika ngoma za mapenzi kupitia mkwaju wake wa kuitwa ‘Teamo’. ‘Teamo’ni moja ya wimbo toka kwenye EP yake ya ‘Sweet Melody’. Ngoma hiyo ambayo imeelekezwa na Hanscana kufikia sasa imeshatazamwa takriban mara thelathini na mbili elfu kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=ocYmfGvwzK8

Soma Pia: Harmonize Atangaza Kuachia Ngoma Mpya Hivi Karibuni

My Queen - Loui Mwanamuziki

Luoi amezidi kuipeperusha bendera ya Bongo Fleva kupitia kazi yake mpya kabisa ya kuitwa ‘My Queen’ ambayo video yake imeachiwa wiki hii. Video hio imefanyika huko visiwani Zanzibar ikiwa ni video ya muziki rasmi ya kwanza kutoka kwa Loui kwa mwaka huu.

https://www.youtube.com/watch?v=0Nkl8FJZiIg

Macho - TID

Fundi wa muziki wa Bongo Fleva TID wiki hii aliachia mkwaju wake wa ‘Macho’ ambao ni maalum kwa wapendanao wote. Hii ni ngoma ambayo kwa mujibu wa msanii huyo inatarajiwa kuwepo kwenye albamu yake ya "Ni yeye" inayotarajia kuingia mtaani hivi karibuni.

https://www.youtube.com/watch?v=6KZTQVrqJ1Qv

Leave your comment