Meneja wa Nandy Azungumzia Madai ya Bifu Kati ya Nandy na Wasafi
13 January 2022
[Picha: EATV]
Mwandishi: Charles Maganga
Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram
Meneja wa msanii Nandy aitwaye Mocco Biashara amekanusha tetesi zilizopo kwa muda mrefu sasa kuwa msanii wake ana mgogoro na kampuni ya Wasafi ya kwake Diamond Platnumz.
Tetesi kuhusu uwepo wa bifu baina ya Nandy na Wasafi zilishika kasi mwaka jana baada ya Nandy kutofanya mahojiano yoyote kwenye kituo cha Wasafi FM pamoja na Wasafi TV vyombo vya habari ambayo vyote zinamilikiwa na Diamond Platnumz.
Soma Pia: Nandy Adokeza Ujio wa Video ya ‘Kunjani’
Pia collabo ya Nandy ya ‘Nibakishie’ aliyofanya na Ali Kiba pamoja na ngoma ya ‘Acha Lizame’ aliyomshirikisha Harmonize ambaye anatajwa kuwa hasimu wa kimuziki wa Diamond Platnumz zilipelekea watu kushuku kuwa huenda mshindi huyo wa tuzo ya Afrima 2021 anashindana na lebo hiyo kubwa barani Afrika.
Akiongea na waandishi wa habari hivi karibuni, Mocco Biashara alitanabaisha kuwa Nandy hana ugomvi wowote na kampuni ya Wasafi na kwamba kwa mwaka 2021, Nandy hakufanya mahojiano kwenye redio nyingi nchini Tanzania na sio Wasafi pekee.
Soma Pia: Nyimbo Mpya: Rich Mavoko Aachia Video ya ‘Sio Leo’
"Wasafi ni nyumbani muziki wetu unalia. Sio tu Wasafi kuna media kibao hatujaenda kufanya Interview kwa sababu tunapishana labda na time. Nadhani muda unaotuhitaji labda wewe ni muda ambao tunakuwa hatupo. Leo hii Wasafi wanasapoti ngoma zangu mimi kwanini nisiende kwenye Interview," alizungumza Mocco Biashara.
Mocco Biashara aliongeza kwa kusema " Mwaka jana Nandy hakwenda Magic FM do you know about that? Lakini do you know Tasa anavyotusapot? Uliza kama Nandy ameenda East Africa mwaka jana lakini unajua mara ngapi East Africa ni nyumbani? Ni kwa sababu ni nyumbani na tunapishana hatuna time."
Akiwa na Nandy, Mocco Biashara ameweza kusimamia vyema muziki wa Nandy kwani meneja huyo ameshiriki katika uandaaji wa tamasha la kimuziki la Nandy Festival, pia chini ya uongozi wa Mocco Nandy ametoa EP zake mbili ambazo ni ‘Wanibariki’ pamoja na ‘Taste’ EP ambazo zimeweza kufanya vizuri sana hapa Afrika Mashariki.
Leave your comment