Nyimbo Mpya: Rich Mavoko Aachia Video ya ‘Sio Leo’

[Picha: Rich Mavoko Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Baada ya subira ya takriban mwezi mmoja sasa, hatimaye Rich Mavoko ameachia video ya ngoma yake pendwa kabisa ya kuitwa ‘Sio Leo’ ambayo amemshirikisha Big Zulu kutokea Afrika Kusini.

Ngoma ya ‘Sio Leo’ iliingia sokoni mwezi Desemba mwaka 2021 na hii ni ngoma ambayo ndani yake Rich Mavoko anamshukuru Mungu kwa matendo yake makuu aliyomtendea na hasa kwa kumtoa kwenye hali duni na kumpatia maisha mema.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Rayvanny Aachia Video ya 'Stay' Akimshirikisha Abby Chams

Ukisikiliza kwa umakini ngoma hii ni dhahiri shahiri kuwa maudhui na ujumbe uliomo unatukumbusha ngoma ya 2019 Ommy Dimpoz ya kuitwa ‘Ni Wewe’ pamoja na ngoma ya Tommy Flavour ya mwaka 2020 ya kuitwa ‘Jah Jah’ ambayo amemshirikisha Ali Kiba.

Video ya ‘Sio Leo’ imefanyika huko nchini Afrika Kusini na hii ni video ambayo imesheheni stori nzuri ambayo bila shaka imerandana vizuri na mashahiri yaliyomo kwenye ngoma hii ambayo Rich Mavoko anaonekana akiimba kwa hisia sana.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Killy Aachia Video ya 'Ni Wewe' Akimshirikisha Harmonize

Aidha, ubora wa picha ambao ni wa viwango vya juu pamoja na mandhari yaliyotumika kwenye video hii ya ‘Sio Leo’ yameifanya kanda hii ambayo ni ya kwanza kwa Rich Mavoko kwa mwaka 2022 kuwa yenye viwango vya juu.

Kufikia sasa, video ya ngoma hii imeshatazamwa mara kumi na tano elfu kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=0dZdNiCgOl8

Leave your comment