Nyimbo Mpya: TID Aachia Ngoma Mpya ‘Macho’

[Picha: Music in Africa]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki kutokea Tanzania TID ameachia ngoma yake mpya kabisa ya kuitwa ‘Macho’.

Kwenye ngoma ya ‘Macho’ TID anamsifia mpenzi wake na kumuaminisha kuwa anampenda na kumkubali sana. Bila shaka hii ni ngoma mahususi kabisa kwa ajili ya wapendanao na watu walioko kwenye mahusiano.

Soma Pia: Lebo Tano Kutoka Tanzania Zinazotarajiwa Kufanya Vizuri Mwaka 2022

"You drive me crazy you're my number one baby nibebe mimi tu wengine usiwabebe ushakuwa wangu we ni wa pekee, we ndo my number one. Kama saluni mama, kama ni gari mama kodi na mavazi," anaimba TID kwenye aya ya kwanza ya wimbo huu.

Ngoma hii imetayarishwa na Mr Simon ambaye ni mojawapo ya watayarishaji wa muziki wakubwa wa muziki nchini Tanzania ambaye kufikia sasa ameshafanya kazi na wasanii wakubwa kama Maua Sama, Harmonize, Abby Chams na Anjella kutokea Konde Gang.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Rayvanny Aachia Video Mpya Ya ‘Rara’

Hii ni ngoma ya kwanza kutoka kwa TID kwa mwaka huu na ngoma hii inatarajiwa kupatikana kwenye albamu ya TID ya kuitwa ‘Ni yeye’ ambayo iko mbioni kuingia sokoni.

https://www.youtube.com/watch?v=f2y8bemYJjw

Leave your comment