Exclusive DJ Mixes and 100% Ad-Free Music!
Nyimbo Mpya: Zuchu Aachia ‘Kitu’
22 December 2021

[Picha: Citi Muzik]
Mwandishi: Charles Maganga
Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram
Mwanamuziki mashuhuri kutokea Tanzania Zuchu ameachia ngoma mpya ambayo ameipa jina la ‘Kitu’ akiwa amemshirikisha Bontle Smith na Tyler Icu
Kwa mara ya kwanza kwenye muziki wake kupitia ngoma ya ‘Kitu’, Zuchu anaimba muziki wa Amapiano ambao kwa sasa umekuwa ni muziki maarufu sana hapa Barani Afrika.
Soma Pia: Nyimbo Mpya: Ibraah na Harmonize Waachia Video ya 'Addiction'
‘Kitu’ ni wimbo ambao Zuchu anatumia lugha ya picha pamoja na lugha ya tafsida kuelezea na kutoa sifa za kidude ambacho amekiita ‘Kitu’ huku akiwa hajaweka bayana ni kitu gani hasa ambacho alikuwa anamaanisha.
Kwenye aya ya pili anasikika zaidi Bontle Smith ambaye anaimba kwa lugha ya kiingereza.
‘Kitu’ ni wimbo wenye kila sifa ya kuitwa ngoma kali ukitegemea kuwa Zuchu ambaye mara nyingi husikika kwenye muziki wa Baibuda na Bongo Fleva, kwenye wimbo huu sauti ya Zuchu imeweza kupita na kudondoka vizuri kwenye mdundo wa Amapiano.
Soma Pia: Nyimbo Tano Zilizofanya Vizuri TikTok Kwa Mwaka 2021
Ikumbukwe kuwa Bontle Smith ameshawahi kufanya kazi na Marioo kwenye ‘Mama Amina’ huku Tyler ICU pia alishiriki kwenye ‘Beer Tamu’ pia ya msanii Marioo.
‘Kitu’ ni ngoma ya nne kutoka kwa Zuchu kwa mwaka huu nyinginezo zikiwa ni ‘Sukari’, ‘Nyumba Ndogo’ pamoja na ‘Yalaaa’ ambayo pia ilifanya vizuri sana ndani na nje ya Tanzania.
Weekly Top 10 songs

Trust No One3:13
chile-one-so-lucky4:02
Kamwambie3:47
Joy Is Coming3:08
Buwooma2:44
Udede Ft Msomali x Malume & Samas Alifata Hela Remix6:34
Msaliti 11:25
Leo3:39
Maringo4:00
NANI ft. Kamanda Pedeshee3:56
Top stories
- The Marathon
25 April
- Who Is Bad Beric
24 April
- Cashout by monyzoh boy
24 April
- MOSS Kay
24 April


Leave your comment