Professor Jay Atoa Ushauri Kwa Wasanii Wanaowadharau Mashabiki Wao

[Picha: Professor Jay Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mmoja kati ya wanamuziki wakongwe zaidi kwenye tasnia ya muziki ya Tanzania Professor Jay ametoa ushauri kwa wasanii ambao wanawadharau mashabiki wao, akisema kuwa msanii hawezi ng’ara bila mashabiki.

Katika ujumbe aliouchapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram, rapa huyo ambaye anaheshimika mno barani Afrika alisema kuwa mashabiki na wanahabari ndio hujenga na kumpa umaarufu msanii.

Soma Pia: Professor Jay Adai Wasanii wa Bongo Wana Upungufu kwenye Ustadi wa Kutunga Nyimbo

Kwa mujibu wa Profesa Jay, sio sahihi wakati msanii anapata mafanikio na kisha baadaye akawadharau mashabiki wake. Professor Jay alisema kuwa mashabiki ndio msingi wa tasnia ya muziki kwani wao ndio wanawajenga na kuwapa wasanii mkate wao wa kila siku.

Aliwashauri mastaa kwenye tasnia ya burudani kuwaheshimu mashabaki na vyombo vya habari.

"Kwenu ndugu Wasanii na Watu maarufu, Mashabiki wenu wanapowapigania, kuwashangilia na kuwasapoti kwa Hali na MALI sio kwamba ni wajinga na wanawashobokea kiasi kwamba mkaanza kujiona nyinyi ndio nyinyi na kuanza kuwadharau, NO!" Professor Jay aliandika mtandaoni.

Soma Pia: Professor Jay Asimulia Sababu ya Diamond Kulia Alipofanya Kazi na Yeye

"Bali kimsingi ni kwamba hawa ndio roho yenu, wanawajenga, kuwakuza na kuwaletea Mkate wenu wa kila siku na kila HESHIMA mliyonayo sasa, So mjifunze kuwaheshimu sana mashabiki, media na wadau, maana bila wao hakuna nyinyi kabisa Nyambaaaf, asanteni sana," Prof Jay aliendelea.

Prof Jay sio msanii mwenye heshima tu bali ni mmoja kati ya wasanii ambao walichonga muziki wa bongo nchini Tanzania. Anafahamika kama mmoja wa waanzilishi wa mtindo huo wa muziki ambao kwa sasa umepata umaarufu mkubwa na kuvuka mipaka ya taifa la Tanzania.

Leave your comment