Nyimbo Mpya: Kayumba Aachia Video ya ‘Mapenzi Yanauma’

[Picha: Ralingo]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki tajika kutokea Tanzania Kayumba hatimaye ameachia video ya wimbo wake ambao unaitwa ‘Mapenzi Yanauma’.

Kayumba ambaye alianza safari yake ya muziki kupitia shindano la kusaka vipaji la Bongo Star Search, ameachia video ya ngoma hii ambayo ni ngoma namba moja kutoka kwenye EP yake ya "Sweet Pain" ambayo iliingia sokoni wiki kadhaa zilizopita.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Diamond Platnumz Aachia ‘Unachezaje’

‘Mapenzi Yanauma’ ni wimbo wa mapenzi ambao ndani yake Kayumba anaugulia maumivu ya moyo baada ya kutendwa na mpenzi wake ambaye alikuwa anampenda sana.

Upande wa video, kama kawaida Kayumba ameweza kufurahisha mashabiki kwani video ya ‘Mapenzi Yanauma’ inaelezea hadithi ambayo yanaendana kabisa na mashahiri ya wimbo ikieleza kuhusu msichana anayeamua kuchukua uamuzi mzito wa kujiua baada ya kubaini kuwa mpenzi wake ana mahusiano ya kimapenzi na ndugu yake wa karibu.

Soma Pia: Rayvanny Atangaza Kushiriki Kwenye Tamasha la Maluma Huko Ulaya

Director Majag ndiye ambaye ameongoza video hii na ameonesha uwezo wake katika kutengeneza video zinazogusa hisia za watazamaji. Hii ni video ya nne kutoka kwa Kayumba kwa mwaka huu, video nyingine kutoka kwa msanii huyu ambazo zimefanya vizuri ni pamoja na ‘Nimegonga Remix’, ‘Mbona Ghafla’ pamoja na ‘Bomba’ ambayo ilitoka Februari mwaka huu.

https://youtu.be/ngHoTiBSBzo

Leave your comment