Rayvanny Atangaza Kushiriki Kwenye Tamasha la Maluma Huko Ulaya

[Picha: Citi Muzik]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki kutokea nchini Tanzania Rayvanny ametangaza kushiriki kwenye tamasha la muziki lilioandaliwa na msanii Maluma ambalo linatarajiwa kufanyika huko barani Ulaya mapema mwaka ujao.

Habari hizi za kusisimua zimefichuliwa na Rayvanny kupitia akaunti yake ya Instagram wakati anaelezea ukubwa wa ngoma ya ‘Mama Tetema’ ambayo amefanya na msanii Maluma kutokea Columbia.

Soma Pia: Matukio 10 ya Kimuziki Yaliyopamba Bongo Mwaka 2021

 "Sijisifii toka tupate uhuru haijawahi tokea wimbo kama huu East Africa Period. Kama unabisha sema wewe upi? Mama Tetema Global way Chui Rayvanny Maluma Meet Me On Papijuancho Tour" aliandika Rayvanny kwenye akaunti yake ya Instagram.

Papijuancho ni jina la ziara ya mwanamuziki Maluma ambayo inatarajiwa kufanyika huko barani Ulaya ikianzia February 24 mpaka April 10 mwaka 2022.

Ziara hio itaanzia kwenye mji wa Zagreb huko Croatia na kisha kuzunguka kwenye nchi kama Austria, Uingereza, Ureno, Ufaransa na kisha kumalizika mji mkuu wa Israel Tel Aviv.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: ‘Sukari’ Zuchu, ‘Baikoko’ Mbosso na Video Zingine kutoka Bongo Zilizotazamwa Zaidi YouTube Mwaka wa 2021

Rayvanny bado hajabainisha kama atashiriki kwenye miji yote au baadhi lakini hii inatarajiwa kuwa nafasi kipekee ya Rayvanny kuweza kutangaza muziki wake kwenye anga za kimataifa.

‘Mama Tetema’ ni ngoma ambayo imepelekea Rayvanny kuweza kuweka rekodi mbalimbali ikiwemo kuwa msanii wa kwanza kutokea Tanzania na Afrika kwa ujumla kutumbuiza kwenye tuzo za MTV EMA ambazo zilifanyika huko nchini Hungary Novemba 14 mwaka huu.

Aidha, kupitia ngoma hii Rayvanny pia alikuwa msanii wa kwanza kutokea Tanzania kuonekana na kung'ara chati za muziki za Billboard Latin baada ya ngoma kufika namba 12 ikiwa ni wiki mbili tangu Rayvanny atumbuize kwenye tuzo za MTV EMA.

Leave your comment