Nyimbo Mpya: Diamond Platnumz Aachia ‘Unachezaje’

[Picha: Nairobi News]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuzuki mashuhuri kutoka Tanzania Diamond Platnumz ameachia wimbo mpya wenye jina ‘Unachezaje’.

Kama jina linavyoasiria, ‘Unachezaje’ ni ngoma ambayo imepambwa na mdundo wa kuchezeka pamoja na mashahiri mepesi.

Soma Pia: Matukio 10 ya Kimuziki Yaliyopamba Bongo Mwaka 2021

Ndani ya ngoma hii, Diamond Platnumz anagusia kwa uchache suala zima la kiki huku kwenye kiitikio cha wimbo kikinogeshwa na neno ‘Unachezaje’ ambalo linarudiwa mara kwa mara.

 "Mfukoni nina jiti (flati), mkononi K Vant, nasikia kumekiki wapi? Nije kujimwaga kati. Ooh haitoshi kalitaka zima hapahapa kaletewa, Ooh my gosh sasa kazima anataka kupepewa," anaimba Diamond kwenye aya ya kwanza.

Mtindo na midondoko ya ngoma hii inashabihiana na ngoma ya ‘Baba Lao’ ambayo aliitoa mwaka 2019 pamoja na ‘Bado Sana’ ambayo alishirikishwa na Lava lava.

Kikubwa hasa ni kuwa ngoma hii inatarajiwa kurindima kwenye matamasha ya Diamond Platnumz kutokana na mdundo pamoja na mashairi ambayo yanashawishi mashabiki kuimba na kuitikia pindi msanii akitumbuiza.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: ‘Sukari’ Zuchu, ‘Baikoko’ Mbosso na Video Zingine kutoka Bongo Zilizotazamwa Zaidi YouTube Mwaka wa 2021

Ngoma hii imetayarishwa na S2kizzy ambaye pia ameshafanya ngoma tofauti na Diamond Platnumz kama ‘Baba Lao’, ‘Far Away’, pamoja na ‘Iyo’ huku maandalizi ya mwisho yakishughulikiwa na Lizer Classic kutokea Wasafi Records.

Hii ni ngoma ya tano kutoka kwa Diamond Platnumz kwa mwaka huu nyinginezo zikiwa ni ‘Kamata’, ‘Iyo’, ‘Naanzaje’ pamoja na ‘Gimmie’ ambayo amefanya na Rema kutokea nchini Nigeria.

https://www.youtube.com/watch?v=RDd71ot_EW0

Leave your comment