Nyimbo Mpya: Stamina Adondosha Video ya Wimbo wake 'Paradiso' amshirikisha Marissa

[Picha: Stamina Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Staa wa mziki wa hip-hop kutoka Tanzania Stamina ameachia video ya wimbo wake 'Paradiso' ambao amameshirikisha Marissa.

‘Paradiso’ ni ngoma namba 12 kwenye albamu yenye jina kama hilo na video hii inakuja ikiwa imeshatimia takribani siku 9 tangu albamu hiyo iliyojengwa kwa ngoma 13 kuingia sokoni.

Soma Pia: Marioo Atangaza Kuachia Albamu na EP Mpya Kwa Pamoja

Ngoma ya ‘Paradiso’ imebebwa na majonzi mazito kutokana na mashahiri yake kuwa ya huzuni sana. Stamina anashuku na kutabiri hali itakavyokuwa siku ya msiba wake huku akisindikizwa na mwanadada Marissa ambaye anatumia mdundo uliotengenezwa na Bear Beatz kuimba kwa uchungu sana kwenye kiitikio.

Kama wimbo ulivyo, video ya ‘Paradiso’ imeweza kuakisi mashahiri ya ngoma hii. Stamina anaonekana akiwa kwenye mabenchi ya kanisa akiimba na baadaye akiwa kwenye jeneza anabebwa kwa ajili ya maziko huku watesi na marafiki zake wakionekana wakiwa kwenye majonzi makubwa sana.

Soma Pia: Gigy Money Atuma Ujumbe Mkali Kwa Mashabiki Wanaomkosoa Vibaya

Ukali wa video hii umechagizwa hasa na namna ambavyo Deo Abel ambaye ndiye aliyeongoza video hii ameweza kutengeneza video ambayo inahuzunisha.

Kuanzia kwa wahusika ambao wameonesha uhalisia kwenye kulia na kuomboleza, mandhari halisi ya msibani pamoja na upweke na majonzi aliyoonesha Stamina wakati anaimba kwenye video, vimetosha kabisa kufanya hii video iwe na upekee mkubwa sana.

Tangu aachie albamu yake, hii ni video ya kwanza kwa Stamina kuachia na inatarajiwa kufanya vizuri hapa nchini Tanzania.

https://www.youtube.com/watch?v=1lLf4MOmDpw

Leave your comment

Top stories

More News