Gigy Money Atuma Ujumbe Mkali Kwa Mashabiki Wanaomkosoa Vibaya

[Picha: The Citizen]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii maarufu nchini Tanzania Gigy Money kupitia ukurasa wake wa Instagam ametuma ujumbe mkali kwa mashabiki wanaomkosoa vibaya, haswaa wale wanaodai kwamba hana kipaji cha kuimba.

Gigy Money kando na kutoa ngoma zinazovuma ambazo zimempa umaarufu, pia ni mmoja wa wasanii wa bongo ambao wameandamwa na utata sana.

Kwenye chapisho ambalo ameliweka mtandaoni, Gigy Money alikuwa na maswali chungu nzima kwa wakosoaji wanaodai kwamba hajui kuimba.

Soma Pia: Wasanii 10 Chipukizi Kutoka Tanzania Waliofanya Vizuri Mwaka 2021

"We kima unaesema Sijui kuimba hii inakuhusu so wanaonipa show ni wajinga?? So nikiwa studio uwaga napenga makamasi??? So, navyocheza nakuimba nakufata steps we bado unaona mm sio sanii??? Nakuaga naenda kufagia uwanja??? So management yangu haina akili?" kipande cha chapisho la Gigy Money kilisomeka.

Gigy Money aliendeleza ujumbe wake kwa kusema kuwa kwa muda fulani amekuwa mtumwa wa ukusoaji mbaya mtandaoni, ila kwa sasa ameamua kuwa huru na hatokubali kufinyiliwa chini tena.

Alisisitiza kuwa wakati wake unakuja na wanaomdharau kwenye sanaa ya muziki watampa heshima.

Soma Pia: Diamond, Rayvannny, Harmonize na Wasanii Wengine Waliotazamwa Zaidi YouTube Tanzania Mwezi Novemba

"Basi na mm msisahau ni Mtanzania huru naweza kuwa huru kwenye misimamo yangu so nawaahidi ipo siku nitakua pale napojiona mimi Nipo , nitafika ata Afrima yawezekana ata BET awards na hio siku Ni mtanieshimu, nakijua uwezo Wangu na kuhusu kuja kucoment msiache kunitia Hasira na mmeweza so Nawahidi Furaha na mshutuko wa bonde la moyo wako" Gigy Money aliandika mtandaoni.  

Leave your comment

Top stories