Wasanii 10 Chipukizi Kutoka Tanzania Waliofanya Vizuri Mwaka 2021

[Picha: Nyimbo Mpya]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Kama kuna mwaka kwenye historia ya muziki wa Tanzania ambao wasanii wapya wamepata nafasi ya kusikika na kuonesha vipaji vyao mbele ya watanzania basi mwaka 2021 umeweza kufanya hivyo vizuri sana.

Kuanzia Januari mpaka Desemba mwaka huu, ifuatayo ni ya wasanii chipukizi 10 kutokea Tanzania ambao wameweza kufanya vizuri:

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Lava Lava ‘Ng’ari Ng’ari, Chege ‘Sinsima’ na Ngoma Zingine Mpya Tanzania Wiki Hii

Anjella

Watanzania walimfahamu baada ya kushirikishwa na Harmonize kwenye ngoma ya ‘All Night’. Toka hapo malkia huyu wa Konde Gang ameachia ngoma tofauti tofauti ikiwemo ‘Kama’, ‘Sina Bahati’ pamoja na ‘Nobody’ ambayo ilivunja ya rekodi ya kutazamwa mara Milioni moja ndani ya siku moja.

Saraphina

 Saraphina alianza kujulikana miaka miwili nyuma baada ya kujirekodi akiimba nyimbo za wasanii wakubwa kama Diamond Platnumz, Rayvanny, Vanessa Mdee na Teni. Mwaka 2021 ndio Tanzania ilimfahamu vyema mwanadada huyu baada ya kuachia ngoma zake kama ‘In Love’, ‘Sitaki Tena’ pamoja na ‘Sio Kitoto’ akiwa ameshirikishwa na wasanii wakubwa kama Chege pamoja na Baddest 47.

Lody Music

Nyota huyu ambaye pia ni mwanachuo alitetemesha Tanzania na ngoma yake ya ‘Kubali’ ambayo imemfanya kufahamika sana na watanzania. Kufikia sasa, ngoma hiyo imeshatazamwa mara Milioni 1.1 kwenye mtandao wa YouTube.

Mac Voice

Tangu ajiunge na Next Level Music, Mac Voice amekuwa msanii mkubwa sana, hasa baada ya kuachia EP yake ya kuitwa ‘My Voice’ ambayo imesheheni ngoma sita. Wiki chache baada ya kuzinduliwa, Mac Voice alitajwa kuwania tuzo za AEUSA kama msanii bora chipukizi.

Soma Pia: Mbosso ‘For Your Love’, Ibraah ‘Addiction’ na Nyimbo Zingine Zinazovuma YouTube Tanzania Wiki Hii

Abby Chams

Akiwa na miaka 18 pekee, Abby Chams ameweza kujijengea jina jema kwenye muziki wa Tanzania kwa kutumia sauti yake ya kuvutia. Chams ameweza kutoa ngoma tofauti kama vile ‘Chapa Lapa’ na ‘Tucheze’. Ngoma yake kubwa kabisa ni ile ya ‘Kings Of Kings’ ambayo amefanya na Darassa.

Ziddy Value

Mwaka 2021 umekuwa ni mwaka wa baraka sana kwa Ziddy Value baada ya kuwa chini ya High Table Sounds ya Barnaba na kutoa EP yake ya kuitwa ‘From The Street EP’.  EP hio imesheheni ngoma nne zenye uzito wa hali ya juu hivyo kumfanya kutambulika kwa uzuri sana na watanzania.

 Hanstone

Baada ya tetesi za muda mrefu kuwa amejiunga na lebo ya Wasafi, ilipofika Oktoba 7 mwaka huu Hanstone alitupilia mbali tetesi hizo baada ya kuachia EP yake ya kuitwa ‘Amaizing’ ambayo imeundwa na ngoma sita. Hata bila kushikwa mkono na lebo yoyote, EP ya Hanstone imefanya vizuri kwenye mitandao mbalimbali ya kutiritisha muziki.

Seneta Kilaka

Watanzania walimfahamu zaidi baada ya Hamisa Mobeto kufanya remix ya ngoma yake ya ‘Ex Wangu’. Kutoka hapo, Seneta Kilaka hajawahi kurudi nyuma kwani mwezi Septemba mwaka huu aliachia EP yake aliyoipa jina la ‘King Of Singeli’ ambayo imezidi kuthibitisha ubora wa Seneta Kilaka kwenye muziki wa Singeli.

Otuck Williams

Otuck Williams amekuwa na mwaka mzuri sana baada ya kuachia EP yake ya ‘Future Memories’ ambayo ameweza kushirikiana na wasanii wakubwa kama Belle 9, hivyo kumfanya kutambulika zaidi na watanzania.

Frida Amani

Mwaka 2021 kipaji cha Frida Amani kilionekana haswaaa kupitia ngoma yake ya ‘Madam President’ ambayo ilisikika kila kona ya nchi hii, na kumpatia ubalozi wa wa kampeni mbalimbali za serikali ya Tanzania.

Leave your comment