Marioo Atangaza Kuachia Albamu na EP Mpya Kwa Pamoja

[Picha: Marioo Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Nyota wa muziki wa bongo Marioo ametangaza kuwa anaenda kuachia albamu pamoja na EP yake kwa wakati mmoja.

Marioo aliweka haya wazi kupitia ukurasa wake wa Instagram ambako alisema kuwa ameandika na kurekodi ngoma mingi sana kufikia sasa.

Kwa mujibu wa Marioo, amependezwa na ngoma zote alizorekodi na hivyo basi anapanga kuziachia zote kupitia albamu na EP, kwani anahofia kuwa huenda zikapitwa na wakati iwapo hatoziachia.

Soma Pia: Harmonize Atangaza Ujio wa Tamasha Lake Litakalofanyika Mapema Mwaka Kesho

Marioo vile vile aliongezea kuwa ana hamu kubwa sana ya kurekodi nyimbo mpya ila ataachia alizorekodi tayari kwanza.

"Nimerekodi nyimbo mingi sana zote kali yaani mpaka nadata. Hizi ngoma zitaoza humu ndani na bado natamani kurecord ngoma mpya. Aisee EP & Album is coming," Ujumbe wa Marioo kwenye Insta Story yake ulisomeka.

Hapo awali, Marioo alipoulizwa sababu ya albamu yake kuchelewa alisema kuwa timu yake ilikumbana na matatizo za kiufundi ila mashabiki watarajie albamu mwishoni mwa mwaka huu au mapema mwaka kesho.

Soma Pia: Wasanii 10 Chipukizi Kutoka Tanzania Waliofanya Vizuri Mwaka 2021

Marioo ni mmoja kati ya wasanii tajika nchini Tanzania ambao walikuwa wametarajiwa kuachia albamu zao mwaka huu, haswaa baada ya yeye kutangaza ujio wa albamu hiyo.

Tukio la msanii kuachia albamu na EP kwa wakati mmoja ni nadra sana. Hii ni kutokana na uwekezaji wa muda na ufundi unaohitajika katika kuandaa nyimbo zote. Marioo ni mmoja wa wasanii wa bongo ambao wamepanda ngazi haraka na kuweza kupata mafanikio makubwa kwenye tasnia ya muziki nchini Tanzania.

Leave your comment

Top stories