Harmonize Atangaza Ujio wa Tamasha Lake Litakalofanyika Mapema Mwaka Kesho

[Picha: Harmonize Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Bosi wa lebo ya Konde Music Worldwide Harmonize ametangaza ujio wa tamasha lake la muziki ambalo litapewa jina la Afro East Carnival.

Harmonize ameweka tangazo hilo wazi kupitia ukurasa wake wa Instagram ambako pia alifichua kuwa tamasha la kwanza litafanyika mnamo tarehe 14 mwezi wa pili mwaka kesho mjini Dar es Salaam.

Soma Pia: Diamond, Rayvannny, Harmonize na Wasanii Wengine Waliotazamwa Zaidi YouTube Tanzania Mwezi Novemba

Jina la tamasha hilo huenda limetokana na albamu ya kwanza ya Harmonize ambayo ilipewa jina la Afro East. Albamu hiyo ambayo ilitoka mapema mwaka jana ilipata mapokezi mazuri na kumuongezea Harmonize mafanikio makubwa kwenye muziki.

Harmonize pia alifichua kuwa tamasha hilo litawahusisha wasanii wakubwa kutoka Afrika Mashariki japo hakuwataja kwa majina.

"Afro East Carnival 14/2/222. Dar es Salaam jiji la makala Amosi. Lets go meet all the biggest East African artists in one stadium," Harmonize aliandika mtandaoni.

Soma Pia: Alikiba Adhibitisha Tamasha Nchini Kenya Kupitia 'Only One King Tour'

Mtindo wa wasanii kukuja na matamasha yao sio mpya nchini Tanzania kwani kunao wasanii ambao kwa sasa wako na tamasha yao.

Kwa mfano, msanii Nandy amejipa mafanikio na umaarufu mkubwa kupitia matamasha yake ya Nandy Festival ambayo hufanyika kila mwaka. Tamasha la Harmonize iwapo litafanyika na lipokelewe vizuri bila shaka litapandisha nyota yake kwenye tasnia ya muziki wa Tanzania.

sasa, Harmonize anazidi kutamba hewani kupitia albamu yake ya pili kwa jina la ‘High School’ ambayo iko na jumla ya nyimbo ishirini.

Leave your comment

Top stories