Nyimbo Mpya: Bright Aachia Ngoma Mpya ‘Mikono Juu’

[Picha: Mwananchi]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki mwenye kipaji cha aina yake kutokea nchini Tanzania Bright ameachia ngoma mpya aliyoipa jina la ‘Mikono Juu’.

Bright ambaye pia ni mtayarishaji bora wa muziki anaachia ngoma ikiwa imeshapita takriban miezi miwili tangu aachie ‘Nakuja Dar’; ngoma ambayo amemshirikisha rapa Stamina.

Soma Pia: Mbosso ‘For Your Love’, Ibraah ‘Addiction’ na Nyimbo Zingine Zinazovuma YouTube Tanzania Wiki Hii

Tofauti kabisa na tulivyomzoea Bright, ngoma ya ‘Mikono Juu’ ina mahadhi ya muziki wa dancehall.

Kwenye wimbo huu, Bright anawahasa watu wafanye starehe na kurahani maisha kwa kwenda klabu na kumbi mbalimbali za kula bata hasa nyakati za usiku.

"One Two wasela kila siku sikukuu hata kama kwenda kwa miguu tunakesha hatulali usiku huu, kwani kuna tatizo na mtu? Hasara roho pesa makaratasi tumia ikuzoee jinafasi. Upoze koo wote tugonge glasi mizuka ikipanda twende kati" anaimba Bright mwanzoni mwa wimbo huo.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Lava Lava ‘Ng’ari Ng’ari, Chege ‘Sinsima’ na Ngoma Zingine Mpya Tanzania Wiki Hii

Ngoma hii imetayarishwa na mwanamuziki Bright mwenyewe akishirikiana na Bear Beatz kutoka Tanzania.

Video ya ngoma hii imefanyika maeneo ya uswahilini ikimuonesha Bright akiwa kwenye maeneo mbalimbali ya mitaa akiwa anacheza ngoma hiyo, ambayo kufikia sasa imeshatazamwa takriban mara themanini na mbili elfu kwenye mtandao wa YouTube.

https://youtu.be/1uDjhWpZ68c

 

Leave your comment

Top stories

More News