Rayvanny Adokeza Ujio wa Kolabo Baina Yake na Justin Bieber

[Picha: Rayvanny Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki nyota kutoka Tanzania Rayvanny amedhibitisha kukamilika kwa kolabo yake na staa wa muziki kutoka Kanada Justin Bieber.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Rayvanny aliweka wazi taarifa hiyo ambayo iliwafurahisha mashabiki wake.

Chui, kama anavyopenda kujiita, hakutoa taarifa zaidi haswaa kuhusu jina ya ngoma hiyo, aina yake au maudhui yaliyomo mle ndani. Vile vile, bosi huyo wa Next Level Music hakusema tarehe kamili ambayo ngoma hiyo itaachiwa.

Soma Pia: Diamond, Zuchu na Nandy Wabwagwa Kwenye Tuzo za AFRIMA

Kwa sasa mashabiki wanasubiri kwa hamu kuona ngoma hiyo haswaa ikizingatiwa kuwa wasanii hawa wawili ni mastaa katika aina tofauti ya miziki wanazofanya. Justin Bieber amejulikana sana kwa mtindo wa RnB huku Rayvanny amejulikana sana kwa mtindo wa bongo.

Bado haijulikani iwapo wasanii hao watajuimuisha mitindo yote. Tangazo hilo lilitokea muda mfupi baada ya Rayvanny kuandikisha historia ya kuwa msanii wa kwanza kutoka Tanzania kutumbuiza kwenye jukwa la MTV EMA.

Soma Pia: Ray C Aomba Serikali Kuingilia Kati Ugomvi Uliopo Baina ya Harmonize na Diamond

Rayvanny alitumbuiza wimbo wa 'Mama Tetema' ambayo ni remix aliyoifanya na msanii kutoka Kolombia Maluma. Hili lilimfanya kupamba vichwa vya habari huku wadau tofauti kwenye tasnia ya muziki wakijitokeza na kumpongeza kwa mafanikio yake.

Nyota yake, hata hivyo, itang'aa zaidi iwapo kolabo hiyo na Justin Bieber itatoka hivi karibuni. Rayvanny ni mmoja wa mastaa wa muziki kutoka Tanzania ambao wamefanikiwa kupanua soko zao za muziki na kufikia dunia nzima.

Leave your comment

Top stories