Diamond, Zuchu na Nandy Wabwagwa Kwenye Tuzo za AFRIMA
22 November 2021
[Picha: Music in Africa]
Mwandishi: Brian Sikulu
Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram
Wanamuziki wa bongo walishindwa kung'aa katika tuzo za AFRIMA (All Africa Music Awards) kwa mwaka 2021.
Hafla hiyo ilifanyika usiku wa tarehe 21 mwezi huu wa Novemba katika hoteli maarufu iitwayo Eko mjini Lagos, Nigeria.
Mastaa wakubwa wakiwemo Diamond Platnumz, Zuchu, Rosa Ree, Nandy na wengine kutoka Tanzania waliteuliwa katika vipengele tofauti vya tuzo hizo.
Soma Pia: Harmonize Aeleza Kwa Upana Sababu ya Mgogoro Baina Yake na WCB
Tofauti na tuzo za awali ambapo wasanii wa bongo hung'aa na kutawala tuzo za AFRIMA haswaa katika vipengele vya Afrika Mashariki, mwaka huu ni mtanzania tu mmoja ambaye alituzwa.
Bendera ya Tanzania ilipeperushwa kwenye tuzo hizo kupitia DJ Sinyorita ambaye alituzwa kwenye kitengo cha 'Best African DJ'.
Diamond Platnumz alikuwa amepigiwa upato mkubwa kwenye kitengo cha 'Best Male Artist in Eastern Africa', lakini Eddy Kenzo kutoka Uganda alishinda tuzo hiyo na kuwabwaga.
Soma Pia: Rayvanny Adokeza Ujio wa Wimbo Mpya na Maluma Baada ya Kuachia ‘Mama Tetema’
Kipengele kingine ambacho kilitawaliwa na watanzania katika uteuzi ni 'Best Female Artist in Eastern Africa'. Tanzania na Kenya ndio mataifa ambayo yalikuwa na idadi kubwa ya wawikilishi kwenye kitengo hiki. Kitengo hiki kilikuwa na wasanii watatu kutoka Tanzania nao ni Zuchu, Nandy na Rosa Ree.
Nikita Kering kutoka Kenya ambaye kwa sasa anavuma na ngoma yake ya 'Ex' ndiye aliyetajwa mshindi wa kitengo hicho. Kwenye tuzo za AFRIMA mwaka jana, Diamond Platnumz alishinda kitengo cha 'Best Male Artist in Eastern Africa' huku Nandy akiibuka mshindi kwenye kipengele cha 'Best Female Artist in Eastern Africa'.
Leave your comment