Director Hanscana Adai Gharama ya Kutengeneza Muziki Imeongezeka

[Picha: Hanscana Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwelekezaji wa video za muziki kutoka Tanzania Hanscana amejitokeza na kudai kuwa gharama ya kutengeneza muziki inazidi kupanda kila kuchao.

Hanscana ambaye ni mmoja kati ya waelekezaji wa video za muziki wanaoheshimika zaidi bongo, na ambaye pia kwa sasa anafanya kazi na lebo ya WCB, alisema kuwa muziki kwa sasa umekuwa biashara mguma sana.

Soma Pia: Babu Tale Akosoa Juma Lokole,Mwijaku na Baba Levo kwa Kuwakashifu Wasanii

Alieleza kuwa licha ya gharama ya utengenezaji wa muziki kuongezeka mno, kipato cha wasanii bado ni kile kile na hakijatingika. Director Hanscana alisema kuwa kuna mambo mbali mbali kama vile kurekodi audio, kurekodi video, kutafutia wimbo soko na kufanya kiki kwa ajili ya umaarufu ambayo yanamgharimu msanii hela nyingi mno.

Aliwashauri wasanii kuwekeza kiakili katika muziki wao na wala sio kuiga wenzao ambao wanafanya makubwa kwenye tasnia ya muziki.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Martha Mwaipaja Aachia Wimbo Mpya ‘Ni Siku Kuu’

"Muziki umekuwa biashara mgumu mno kwa upande wa mapato kwa wasanii so wekezeni kiakili sio kimkumbo," ujumbe wa Hanscana kwenye mitandao ya kijamii ulisomeka.

Hanscana alionekana kusikitishwa na jinsi tasnia ya burudani imebadilika Tanzania. Alisimulia jinsi wasanii walihitajika mno katika sehemu za burudani kwa enzi za kale, ila kwa sasa sehemu hizo hujaa bila ata ya wasanii kuwepo.

Kwa mujibu wa Hanscana ma DJ wameonekana kuchukua nafasi ya wasanii. "Zamani club hazijai bila msanii kuwepo ila now days sehem za starehe zinajaa kwa dj'z tu yani dj'z wanashows nyingi kulipo wasanii ," Hanscana aliandika mtandaoni.

Leave your comment