Babu Tale Akosoa Juma Lokole,Mwijaku na Baba Levo kwa Kuwakashifu Wasanii

[Picha: The Star]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Babu Tale ambaye ni meneja wa mwanamuziki nyota Diamond Platnumz amejitokeza na kuwakashifu watu maarufu ambao wanawakosoa vibaya wasanii wa bongo.

Kupitia mahojiano aliyoyafanya hivi karibuni, Babu Tale alidai kuwa wakosoaji hao wanachangia katika kuwafisha moyo wasanii na hivyo basi kwa kiasi fulani kuchangia katika kuua muziki wa bongo.

Soma Pia: Alikiba Atangaza Ujio wa ‘Only One King’ Tour

Bila ya kuponza maneno yake, Babu Tale aliwataja wazi wanahabari wakubwa Tanzania ikiwemo Juma Lokole, Mwijaku na Baba Levo ambao wanajulikana kwa ukusoaji wao mkali dhidi ya wasanii fulani.

Alisisitiza kuwa wasanii wanafaa kushawishiwa kufanya vizuri na wala si kukwazwa na dhana ambazo zinawafinyilia chini.

Babu Tale ambaye pia ni mlezi wa vipaji vya wasanii alisema kuwa iwapo angekuwa na nguvu angewatoa wakosoaji hao kwenye tasnia ya muziki wa bongo.

Soma Pia: Harmonize na Anjella Washirikishwa Kwenye Albamu Mpya ya DJ Neptune

"Tupinge hawa wagomabanishi wachache, Mwijaku, Baba Levo, huyu Juma Lokole, hawa ndio wapumbavu. Tuwatoe hawa kwenye hii industry yetu. Tu support muziki wetu. Na wewe ukishika mic ukiendeleza hiyo dhana, tunaendelea kuua muziki. Tuwache hiyo dhana," Babu Tale alieleza.

Kando na ukusoaji wa wasanii, Babu Tale vile vile alizungumzia suala la mafanikio ya wasanii kutokana na ukubwa wa lebo walikosaniwa. Alieleza kuwa si lazima msanii awe kwenye lebo tajika ndio aweze kuvuma na kutoa ngoma nzuri.

Alitoa mfano wa msanii chipukizi ambaye anaitwa Lody Music, na kueleza kuwa licha ya yeye kutotoka katika lebo kubwa tajika Tanzania, muziki wake ulikuwa umekubaliwa na mashabiki.

Leave your comment