Nyimbo Mpya: Martha Mwaipaja Aachia Wimbo Mpya ‘Ni Siku Kuu’

[Picha: Gospoa]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Gwiji wa muziki wa Injili kutokea nchini Tanzania Martha Mwaipaja amerudi tena na wimbo mpya wa kuabudu unaoitwa ‘Ni Siku Kuu’.

Huu ni wimbo ambao Martha Mwaipaja anaonesha ni namna gani ambavyo anasubiri kwa hamu siku ambayo atafika kwenye uzima wa milele na kuoshwa makosa na dhambi zote.

Soma Pia: Alikiba Atangaza Ujio wa ‘Only One King’ Tour

Kupitia wimbo huu, Martha anaonesha tumaini na hamu ya kufika kwa siku hiyo. Martha anaimba peke yake kwa sauti ya utulivu kwenye aya ya kwanza akisema "Ni sikukuu siku ile ya kumkiri mwokozi moyo umejaa tele kunyamaza hauwezi."

Kwenye aya ya pili Martha anaendelea kuimba huku akisindikizwa na vyombo vya muziki kama kinanda na gitaa na mwishoni mwa aya hii ya pili ndipo Martha Mwaipaja anapewa msaada wa sauti na waimbaii wengine ambao sauti zao zinasikika pia.

Soma Pia: Harmonize na Anjella Washirikishwa Kwenye Albamu Mpya ya DJ Neptune

Wimbo huu umelenga kutoa faraja na tumaini kwa watu wote kuwa ipo siku machozi yao yatafutwa na makosa kuwekwa kando itakapofika hiyo ‘Siku Kuu’

’.

Video ya wimbo huu imeakisi mazingira ya utulivu kama ambavyo wimbo ulivyo na Martha anaonekana akiwa anaimba kwa hisia kwenye maeneo tofauti tofauti akiwa ameketi na kusimama na bila shaka hii ni video ambayo imetulia na itakufanya utulie.

https://www.youtube.com/watch?v=kPsxcybS4R8

Leave your comment