Video ya ‘Zai’ ya Maua Sama Kuwania Tuzo Uholanzi

[Picha: YouTube]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki kutokea nchini Tanzania Maua Sama amepiga hatua nyingine kwenye muziki wake baada ya video yake ya ’Zai’ kutajwa kuwania kwenye tuzo za New Vision International Awards ambazo hufanyika huko Uholanzi.

Maua Sama kupitia akaunti yake ya Instagram alitoa taarifa hizo kwa mashabiki zake na kudokeza kuwa huenda akaenda kwenye tuzo hizo ambazo zinatarajiwa kufanyika huko Amsterdam Uholanzi Desemba 20 mwaka 2021.

Soma Pia: Maua Sama Aweka Wazi Mipango ya Kufungua Lebo Yake ya Muziki

"Amsterdam see you soon. ZAI Nominated Best Music Video - New Vision International Awards. Asanteni kwa kuendelea kusupport muziki mzuri hii inakuja nyumbani asubuhi mapema, Nawapenda sana," aliandika Maua Sama.

Maua Sama aliachia video ya ‘Zai’ Oktoba 20 mwaka huu na tangu kuachiwa kwake, video hio imekuwa ni video pendwa baina ya mashabiki.

Kilichovutia hasa ni namna ambavyo video hiyo imeonesha uhalisia wa maisha ya uswahilini. Kumtumia Hakika Reuben ambaye ni mchekeshaji machachari sana Tanzania imechangia kufanya video hii kuwa bora sana.

Soma Pia: Maua Sama Aeleza Maoni Aliopata Kutoka kwa Mwana Fa Kabla ya Kutoa Ngoma ya ‘Zai’

New Vision International Awards ni tuzo ambazo zilianza mwaka 2018 huko nchini Uholanzi na zina lengo la kukuza, kuhamasisha na kuheshimisha kazi zote zinazofanyika kwenye kiwanda cha filamu sehemu mbalimbali duniani huku kazi zote ambazo huteuliwa kuwania tuzo hizo huchaguliwa kwa kuzingatia ubora na uhalisia wa kazi.

https://www.youtube.com/watch?v=MAmFhxxGJoc

Leave your comment