Professor Jay Apongeza Wasanii wa Kenya Kwa Kutetea Haki Zao
18 November 2021
[Picha: Instagram]
Mwandishi: Charles Maganga
Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram
Rapa kutokea nchini Tanzania Professor Jay amewapongeza wasanii kutokea Kenya katika harakati zao za kupinga wasanii wa nje kulipwa zaidi kuliko wasanii wazawa wa nchi hiyo.
Akiongea kwenye kipindi cha ‘Amplifaya’, Profesor Jay ametoa pongezi nyingi kwa wasanii kutokea Kenya kwa kutaka mabadiliko. Pia alitumia mahojiano hayo kutaka mamlaka husika kutengeneza sheria ambazo zitasaidia kukuza vipaji kutoka Tanzania.
Soma Pia: Professor Jay Adai Wasanii wa Bongo Wana Upungufu kwenye Ustadi wa Kutunga Nyimbo
"Kwanza niwape big up sana wasanii wa Kenya kwa kupata mwamko huo. Kwa mfano sasa hivi Tanzania kwenye clubs na maeneo mbalimbali ya starehe wanamuziki kutokea nchini South Africa wamechukua nafasi kubwa sana kiasi kwamba local content haizingatiwi sana," alisema Professor Jay.
Professor Jay amedokeza pia kwamba Tanzania inatakiwa itunge sheria ya Afrika Kusini ambayo imetoa nafasi kwa nyimbo za nchini humo kusikilizwa zaidi kuliko nyimbo za wasanii kutokea nchi za nje.
Soma Pia: Professor Jay Afichua Sababu ya Uhasama Baina ya Wasanii wa Kizazi Kipya na Cha Kale
"Wakati huo tunacheza ngoma kutoka South Africa wenyewe wana ile sheria yao ambayo imepitishwa kusimamia local content yao labda wacheze muziki kutokea South Africa labda asilimia 90 au asilimia 85 alafu muziki mwingine kutokea maeneo mengine uchezwe kwa asilimia zilizobaki," alizungumza msanii huyo.
Leave your comment