Nyimbo Mpya: Professa Jay Aachia ‘Shikilia’ Akiwashirikisha Maua Sama na Young Lunya

[Picha: YouTube]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Nguli wa muziki wa Hip-hop nchini Tanzania Professa Jay ameachia video ya wimbo wake wa ‘Shikilia’ ambao amemshirikisha Maua Sama na Young Lunya.

Pamoja na kwamba ni ngoma ya Hip-hop, video ya ‘Shikilia’ itakufanya uchangamke kutokana na mitindo mbalimbali ya dansi iliyotumika kwenye video hii.

Soma Pia: Maua Sama Azungumzia Uhusiano Wake Na Nandy

Mandhari yaliyotumika kwenye video kama club na fukwe za starehe imethibitisha kabisa kwamba watayarishaji wa video hii walilenga kuchangamsha zaidi watazamaji.

Aidha, namna ambavyo Professa Jay amejiachia na kuvaa uhusika wa mwanaume ambaye anapenda sana kwenda sehemu za starehe na kula bata ni kitu kingine cha kupongezwa na kupigiwa makofi.

Soma Pia: Maua Sama Ataja Changamoto Alizopitia Katika Kuandaa Video ya ‘Zai’

Kazi hii imetukumbusha Professa Jay wa enzi za ‘Kamili Gado’, video ambayo ilifanya vizuri pia miaka kadhaa nyuma.

Kazi ya kutengeneza video hii amekabidhiwa Director Hanscana ambaye ni nguli wa kutengeneza video za muziki nchini Tanzania, na ana wasifu wa kufanya kazi na wasanii kama Diamond Platnumz, Alikiba, Harmonize, Rayvanny na wengineo wengi.

Ngoma hii ilitoka siku kadhaa nyuma na iliandaliwa na Bin Laden. Hii ni ngoma ya pili kwa mwaka huu kuwakutanisha Maua Sama na Young Lunya kwani kabla ya hapo, wawili hao walifanya ngoma ya ‘Away’ iliyotoka wiki kadhaa nyuma.

https://www.youtube.com/watch?v=BvY-eI3y_4g

Leave your comment