Nyimbo Mpya: Jay Melody Aachia Video ya ‘Halafu’

[Picha: YouTube]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki shupavu toka Tanzania Jay Melody ameachia video ya wimbo wake ‘Halafu’.

Video ya ‘Halafu’ inakuja miezi miwili tangu Jay Melody aachie audio ya wimbo huo iliyotayarishwa na nguli wa kutengeneza ngoma za muziki wa Bongo Fleva Genius Jini.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Jay Melody Aachia Ngoma Mbili ‘Halafu’ Na ‘Sambaloketo’

Kama ilivyotarajiwa, maudhui ya video ya ‘Halafu’ yamerandana kabisa na kilichoimbwa kwenye wimbo ambapo ndani ya video kuna stori ya namna ambavyo Jay Melody alivyokuwa anateswa kimapenzi na mwenza wake wa zamani.

Vilevile kwa kuwa ni wimbo wa kuchangamka, Kuna mitindo mbalimbali ya dansi ambayo imetumika kuchangamsha video.

Soma Pia: Jay Melody Azungumzia Ripoti Kuwa Amejiunga na Lebo ya Rayvanny Next Level Music

Uzuri wa video hii ni namna ambavyo Kelly Film ambaye ndiye mtayarishaji wa video hii ameweza kutumia wahusika kuleta hadithi nzuri ambayo imejawa na vichekesho na mafundisho.

Vitu vingine kama ubora wa picha, mandhari na hata mavazi nadhifu ya Jay Melody yameongezea nakshi video hii.

 Kwa Jay Melody, ‘Halafu’ ni video ya nne yeye kuiachia kwa mwaka huu. Kabla ya hapo, aliwaburudisha watanzania kupitia video za nyimbo kama ‘Huba hulu’, ‘Najieka’ pamoja na ‘Sambaloketo’ na zote zilifanya vizuri.

https://www.youtube.com/watch?v=HK0wy5zsGec

Leave your comment