Nyimbo Mpya: Jay Melody Aachia Ngoma Mbili ‘Halafu’ Na ‘Sambaloketo’

[Picha: Mzigo TV]

Mwandishi: CHarles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msani tajika kutoka Tanzania Jay Melody ameachia nyimb mbili mpya ‘Halafu’ na ‘Sambaloketo’.

Jay Melody ambaye anasifika kwa kipaji chake cha uandishi ametoa nyimbo hizo ambazo ameshirikisha watayarishaji wa muziki wawili tofauti.

Soma Pia: S2kizzy: ‘Tetema’ ya Rayvanny Ndio Wimbo Ulioniletea Mafanikio Zaidi

Tukianza na ‘Halafu’, Jay Melody kwenye wimbo huu anaringa na kutamba huku akimsimulia mpenzi wake wa zamani namna ambavyo anafurahi na kurahani kwenye penzi lake jipya.

 "Eti unataka nini hivo naambiwa mimi kimahaba kama jini. Yani moto hauzimi uko nyuma nilipata varangati ni mateke kama sensia Ex kazi yako kuumia," anaimba Jay Melody kwenye mojawapo ya mistari ya wimbo huo.

‘Halafu’ umetayarishwa na Jini X 66 ambaye pia ndiye alihusika kutayarisha na kutengeneza  ‘Huba Hulu’ na ‘Najieka’.

Kwenye wimbo wa ‘Sambaloketo’ ambao umetayarishwa na Mr LG, Melody anapita kwenye mdundo ambao umetumia vionjo vya nyimbo za zamani. Kimaudhui, wimbo huu ni wa kimapenzi ambapo Jay Melody anaonesha jinsi mwandani wake anavyompa mapenzi mazito.

Soma Pia: Zuchu Ajibu Madai ya Uhasama Baina Yake na Queen Darleen

Jay Melody kwenye aya ya kwanza anaimba "Ooh My baby nzela wa zoro nipe akapela nipone huo moyo sambaloketo."

Nyimbo hizi mbili zinakamilisha idadi ya nyimbo nne kutoka kwa Jay Melody ndani ya mwaka mmoja na mpaka sasa nyimbo hizi mbili bado hazijatoka video na bila shaka mashabiki watakuwa wanasubiria kwa hamu.

https://www.youtube.com/watch?v=f2jLYVJXfZ4

Leave your comment