Zuchu Ajibu Madai ya Uhasama Baina Yake na Queen Darleen

[Picha: Queen Darleen Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Lebo ya WCB inasifika sana kwa mafanikio yake makubwa na pia uwezo wa kuwatoa wasanii wenye ushawishi. Takriban wasanii wote walioko WCB au wenye walipitia katika lebo hiyo wapo miongoni mwa wasanii tajika Tanzania.

Kwa muda mrefu, msanii Queen Dareen ndiye aliyekuwa mwanamuziki wa kike pekee yake katika WCB hadi mwaka jana amabpo lebo hio ilimzindua Zuchu.

Soma Pia: Zuchu Afichua sababu ya Maua Sama, Nandy kukosa Kwenye Tamasha la Zuchu Homecoming

Baada ya kuzinduliwa na kupata umaarufu mkubwa, tuhuma ziliibuka mtandaoni zikiashiria kuwa Queen Darleen na Zuchu walikuwa na uhasama baina yao. Kulingana na tuhuma hizo zilizovujwa mtandaoni na Don Dada Masha, wasanii hao wawili hawakuwa katika hali nzuri ya kiurafiki.

Zuchu na Queen Darleen walibaki kimya kuhusu taarifa hizo licha ya tuhuma kuenea na kukita mizizi katika mitandao ya kijamii. Kwa mara ya kwanza, Zuchu amelizungumzia suala hilo na kubaini ukweli wa mambo.

Soma Pia: Zuchu: Vannessa Mdee Aliwacha Pengo Kubwa Baada ya Kujitoa Kwenye Muziki

Zuchu kwanza aliweka wazi kuwa yeye ni rafiki wa karibu wa Queen Darleen na hapajawahi tokea uhasama baina yao. Pia aliongeza kuwa wakati tuhuma hizo ziliibuka mtandaoni, Queen Darleen alimpigia simu na wakaongea.

Zuchu alisema kuwa tuhuma hizo hazikuwa za ukweli na Masha ambaye ndiye aliwasha moto tayari alikwisha omba msamaha kwake Queen Darleen.

"Queen Darleen sijampunguzia kasi, tupo wote hata kwenye hii show ya Zanzibar atakuwepo. Juzi tu alikuwa nyumbani kwangu tumekaa tumepiga story, tuko vizuri naomba mtuache," Zuchu alisema.

Leave your comment