Zuchu: Vannessa Mdee Aliwacha Pengo Kubwa Baada ya Kujitoa Kwenye Muziki

[Picha: Nairob Wire]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii wa WCB Zuchu amejitokeza na kusema kuwa Vanessa Mdee aliwacha pengo kubwa sana katika tasnia ya muziki ya Tanzania. Akizungumza katika mahojiano na Wasafi TV, Zuchu alisisitiza kuwa Mdee alikuwa msanii mwenye hadhi ya juu katika muziki wa bongo.

Soma Pia: Wasifu wa Vanessa Mdee, Nyimbo Zake Bora, Tuzo Alizoshinda, Mahusiano na Thamani Yake

Vanessa Mdee ambaye alikuwa msanii mwenye ushawishi mkubwa ndani na nje ya Tanzania alichia ngoma zilizovuma katika anga za burudani.

Ushawishi wake na ubora wake kimuziki ulimfanya akawa mmoja wa majaji katika East Africa Got Talent. Mwaka jana, alitangaza kuacha muziki. Tangazo hilo lilikuwa pigo kubwa kwa tasnia ya muziki ya Tanzania, haswaa ikizingatiwa kuwa Vanessa Mdee alikuwa mmoja wa mwanamuziki wa kike aliyekuwa akifanya vizuri sana.

Soma Pia: Wasifu wa Nandy, Nyimbo Zake Bora, Tuzo Alizoshinda, Mahusiano na Thamani Yake

Zuchu alisema kuwa chuki na uhasama ndio ugonjwa unaoathiri tasnia ya muziki Tanzania. Alieleza kuwa yafaa kuwe na upendo baina ya wasanii na kuungana mkono kusudi kuijenga tasnia ya burudani.

Zuchu alikuwa akijibu swali kuhusu tuhuma za yeye kuchukiwa na kuonewa gere na wanamuziki wenzake wa kike kutokana na mafanikio yake makubwa.

"Tulikuwa naye Vanessa Mdee, leo ameondoka tunaona pengo lake kubwa. Yaani ameacha bonge la gap kwa sababu kipindi Vanessa yupo, we would still talk like this about her. Tulikuwa tunamwona kwa stages ambazo hatukutegemea wasicha wa kitanzania kufika ambayo alifika," Zuchu alisema.

Leave your comment