Zuchu Afichua sababu ya Maua Sama, Nandy kukosa Kwenye Tamasha la Zuchu Homecoming

[Picha: Zuchu Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

 

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki maarufu kutoka mkoa wa Zanzibar Zuchu amefunguka kuhusu kukosekana kwa wasanii Maua Sama na Nandy kwenye tamasha lake lijalo la Zuchu Homecoming.

Tamasha hilo litafanyika mnamo tarehe 21 mwezi huu katika uwanja wa Amani mkoani Zanzibar.

Soma Pia: Nandy Afafanua Madai ya Kusainiwa na Lebo ya Mr. Eazi

Kwa wiki kadhaa sasa, Zuchu amekua katika shughuli za kufanikisha tamasha hilo. Mojawapo ya suala kuu ambalo Zuchu amewekeza muda mwingi sana ni orodha ya wasanii watakao tumbuiza mashabiki siku hiyo.

Kando na kuwa na wasanii chipukizi, Zuchu pia ataandamana na wasanii waliobobea bongo. Baadhi ya wasanii watakaokuwepo ni pamoja na Lulu Diva, Jux, Gigy Money, Dula Makabila, Khadija Kopa pamoja na wengine wengi.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Mbosso Aachia Video Mbili ‘Your Love’ na ‘Tulizana’

Kwenye orodha hiyo hapakuwepo Nandy na Maua Sama, na hili limekua suala ambalo limezua gumzo sana mtandaoni. Akizungumza katika mahojiano na wasafi TV, Zuchu alieleza sababu ya wasanii hao kukosekana kwenye tamasha lake. Alisema kuwa baadhi ya wasanii waliopigiwa simu kama vile Maua Sama watakuwa na shughuli nyingine zao kibinafsi siku hiyo ya tamasha.

Alieleza zaidi kuwa yeye pamoja na timu yake walijaribu kadri wawezavyo kuchagua wasanii bora watakaotumbiza.

"Nadhani wengine ni schedule zao. So far mimi nliiachia timu maalum ndio walikuwa wana approach wasanii. Wasanii wachache sana nili waa aproach mimi mwenyewe. Kwa hivyo kama Maua nilimpigia mimi mwenyewe, kwa bahati mbaya Maua atakuwa na kazi," Zuchu alieleza.

Leave your comment