Nandy Afafanua Madai ya Kusainiwa na Lebo ya Mr. Eazi

[Picha: Mr Eazi Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii tajika kutoka Tanzania Nandy amejitokeza na kufafanua uhusiano wake kama mwanamuziki na kampuni ya Empawa inayomilikiwa na Mr. Eazi kutoka Nigeria. Hapo awali, habari zilisambaa mtandaoni kuwa Nandy alikuwa amesainiwa kwenye lebo ya Mr Eazi.

Hii ilikuwa baada ya Mr. Eazi kukutana na Nandy na kisha baadaye kumkaribisha kwenye Empawa. Katika taarifa aliyochapisha mtandaoni, Nandy aliweka wazi kuwa hakuwa amesainiwa katika lebo yoyote.

Soma Pia: Nandy Atangaza Kolabo Mpya Na Sho Madjozi

Aliongezea kuwa yeye ni msanii huru anayejitegemea tofauti na habari zilizokuwa zikisambaa mtandaoni. Hata hivyo, Nandy alieleza kuwa uhusiano ulipo baina yake na Mr. Eazi ni wa biashara tu.

Kulingana na Nandy, kuna mambo mengi sana hufanyika katika utengenezaji wa muziki unaohitaji kuhusisha watu mbali mbali. Aliweka kuwa yeye na Mr Eazi wamekuwa washirika wenza katika biashara kwa muda sasa. Nandy aliwashauri watu kupuuza habari bandio zilizoko mitandaoni.

Soma Pia: Nandy: Ilinigharimu Milioni 40 Kufanya Wimbo wa ‘Leo Leo na Koffi Olomide

"Mimi na Mr Eazi ni business partners sio kwenye mziki tu hata biashara sababu kutoa mziki kuna vitu vingi nyuma ya mziki wetu!! Maswali yamekuwa mengi sana page zinaandika sana mara nime sainiwa mara ivi mara vile noo guys me ni msanii ninaye jitegemea na kushirikiana na wafanya biashara wenzangu. punguzeni habari fake," Nandy aliandika mtandaoni.

Ni muhimu kukumbuka kuwa kampuni ya Empawa si lebo ya kurekodi muziki kama vile wanavyofikiria wengi, bali ni kampuni inayohusika na usambazaji wa muziki.

Leave your comment